Na Daudi Manongi,MAELEZO.
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli
Nchini (TPDC) limekabidhi msaada wa Viti 142 kwa shule ya Sekondari
Kisungu iliyopo Tabata Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi msaada huo leo Jijini
Dar es Salaam Meneja Mawasiliano wa TPDC alisema taasisi hiyo imeamua
kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Mhe.John Pombe Magufuli za kupunguza uhaba wa madawati katika shule
za Msingi na Sekondari nchini.
“TPDC inaunga mkono jitihada za
Rais John Pombe Magufuli katika kumaliza tatizo la wanafunzi kukaa
chini, tumeamua kutekeleza kwa vitendo jitihada hizo” alieleza Msellemu.
Aidha Msellemu alisema kwa kipindi
kirefu TPDC imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia huduma za kijamii
nchini ikiwemo elimu na afya, ambapo hivi karibuni taasisi hiyo ilijenga
zahanati pamoja na kukabidhi Madawati 500 katika kata ya Madimba
iliyopo Mkoani Mtwara.
Akipokea msaada wa viti hivyo,
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisungu, Mkamo Mgeta aliishukuru TPDC kwa
msaada ambao umelenga kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli na kuwataka wadau zaidi
kujitokeza kusaidia uhaba huo


No comments:
Post a Comment