KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 20, 2016

ANAYEMFAHAMU MGONJWA HUYU AFIKE MUHIMBILI

ms
Mgonjwa ambaye majina yake hayafahamiki amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali na kujeruhiwa sehemu ya kichwani.
 
Mgonjwa huyu alifikishwa katika hospitali hiyo tarehe 25-09-2016 akitokea Hospitali ya Vijibweni jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa fomu namba tatu ya polisi (PF3), mtu aliyegonga alikimbia.
 
Mgonjwa huyo hawezi kuzungumza na anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo. Mgonjwa amelazwa Kibasila, wodi namba tisa. Endapo kuna mtu au ndugu anamfahamu mgonjwa huyu afike Muhimbili ofisi ya Ustawi wa Jamii au Ofisi ya Uhusiano Muhimbili.

No comments:

Post a Comment