Na: Frank Shija, MAELEZO
UZALENDO umewapatia ajira
takribani vijana 70 baada ya Amiri Jeshi Mkuu,na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufurahishwa na namna
ambavyo washiriki wa zoezi la Amphibia Landing walivyoonyesha umahiri wao.
Hayo yamebainika jana katika
fukwe za kijiji cha Baatani, wilayani Bagamoyo, wakati wa hafla kufunga
mazoezi hayo ambapo Mhe. Rais Magufuli alisema kuwa kutokana na
alivyojionea mazoezi hayo na amearifiwa kuwa kati ya washiriki wa
mazoezi hayo wamo mgambo 30 na JKT 40 aliagiza wote waingizwe kwenye
orodha ya waajiriwa wapya wa JWTZ.
“Katibu Mkuu Kiongozi nakuagiza
ufanya utaratibu wakuwaingiza kwenye ajira hawa vijana 30 wa mgambo na
40 wa JKT kwani wameonyesha moyo wa uzalendo kwelikweli, tena
ikiwezekana ata kesho waingie kwenye orodha ya waajiriwa wapya”. Alisema
Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amemuagiza
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange
kuangalia namna ya kuwapa motishi wote walioshiriki kufanikisha zoezi
hilo ili kuwaongezea morali ya kuwajibika.
Katika hatua nyingine ametoa wito
kwa Majeshi kushirikia hususan katika eneo la unzanzishaji wa viwanda
ili kutoa mchango wao katika hasma ya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
“Ni lazima sasa tujipange nataka
Majeshi yetu muwekeze katika viwanda iwe kwa kuunganishwa nguvu pamoja
ama mmoja mmoja naamini hatushindwi, leteni mpango Serikali itasaidia”.
Alisema Rais Magufuli.
Alitolea mfano wa Jeshi la
Magereza kuwa na kiwanda cha viatu katika Gereza la Karanga mkoani
Kilimanjaro, kushangaa kuona majeshi mengine yananunua viatu kutoka nje
ya nchini. Aliwaagiza washirikiane katika kuhakikisha wanafikia malengo
ya kuwa na viwanda.
Alisema kuwa Jeshi letu limekuwa
na mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu yake ambayo aliyataja
kuwa ni ulinzi wa mipaka ya nchi, kulinda katiba ya nchi, kufundisha
wananchi masuala ya ulinzi wa Taifa, uokoaji na utoaji wa misaada katika
maafa, kutoa elimu ya kujitegemea pamoja na ulinzi wa amani na
ukumbozi.
Nakuongeza kuwa limeweza kulinda
mipaka ya nchi, na kulinda amani iliyopo pamoja na kushirikiana na
Umoja wa Mataifa katika kulinda amani katika baadhi ya maeneo ikiwemo
Sudan Kusini na DRC Congo.
Septemba Mosi mwaka huu JWTZ
walitimiza miaka 52 ya uhai wake,ambapo ilianza kuadhimsha miaka hiyo
kwa kufanya shughuli mbalimbali kama vile usafi, huduma za upimaji wa
Afya Bure na zoezi hili la Amphibia Landing ni muendelezo wa maadhimisho hayo.
Ambapo katika zoezi hilo vifaa
kama Meli Vita, Vifaru vinavyo tembea nchi kavu na majini, milipuko
pamoja na Ndege vita vilitumika.
No comments:
Post a Comment