
Mbunge wa Vijana kutoka Mkoa wa Kigoma, Mh.Zainabu Katimba.
…………………………………………………………………..
Na Emmanuel Matinde-Kigoma
VIJANA wametakiwa kufuata
mafundisho ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, juu
ya uwajibikaji katika kazi,kuwa wazalendo, kudumisha amani na kuwa
walinzi wa amani ya nchi yao.
Mbunge wa Vijana kutoka Mkoa wa
Kigoma, Mh.Zainabu Katimba, metoa wito huo juzi katika kijiji cha
Katanga wilayani Kakonko, mkoani Kigoma, wakati akihitimisha ziara yake
ya siku tatu mkoani humo katika siku ya kumbukumbu ya miaka 17 tangu
kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema wakati wa uhai wake
Mwalimu alihubiri uwajibikaji, uzalendo, amani na upendo na kupinga
rushwa, hivyo vijana wana wajibu wa kuyazingatia yote hayo kwa manufaa
ya taifa.
“Tuendelee kufanya kazi ili kumuenzi mwalimu kama vile rais wetu Magufuli anavyofanya kwa vitendo,”alisea Mh.Zainabu.
Kuhusu suala la amani Mh.Zainabu,
ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Chipukizi Sekondari na vyuo vikuu,
alisema vijana hasa waishio mpakani na nchi jirani wanalo jukumu kubwa
la usalama wan chi yao kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na kutoa
taarifa pindi wanapoona watu wanaowatilia mashaka.
Kauli ya mbunge huyo inakuja siku
moja tu baada ya askari polisi wakishirikiana na askari wa jeshi la
wananchi kuwaua majambazi wawili waliokuwa wanajiandaa kufanya uhalifu
katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko baada ya kukabiliana nao kwa
risasi.
Nao baadhi ya vijana katika
kijiji cha Katanga wakiwemo Nestory John na Honorata Petro, walieleza
utayari wao katika kuhakikisha kwamba wanafichua mtu yeyote mwenye nia
ya kuhatarisha usalama katika maeneo yao.
Katika ziara yake Mh.Zainabu
Katimba, alilenga kukutana na vijana, kusikiliza changamoto zao na
kuhamasisha vijana kuanzisha na kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali
na yeye kuahidi kushirikiana nao ili kupata fedha za kuanzisha miradi
ya ujasiriamali ikiwemo asilimia 5% ya fedha zitolewazo na halmashauri
kwa ajili ya vijana.
Vile vile alitoa kiasi cha
shilingi milioni mbili kwa ajili ya kuwezesha usajili wa vikundi 18 vya
vijana katika wilaya za Kigoma vijijini, Buhigwe, Kasulu, Kibondo na
Kakonko.


No comments:
Post a Comment