WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amekutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya CRCC ya China Bw.
Fengchao Meng ambaye ameahidi kuwekeza kwa kushirikiana na Serikali
katika kuboresha miundombinu ya mkoa wa Dodoma.
Mwenyekiti huo ambaye aliongozana na Mwenyekiti wa Kampuni nyingine ya Ujenzi ya CCECC ya China, Bw. Yuan Li pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki kati ya Serikali za Tanzania na China, Bw. Joseph Kahama .
Akizungumza na Bw. Meng leo
(Jumatatu, Oktoba 10, 2016) ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam,
Waziri Mkuu amesema kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni uendelezaji wa
Makao Makuu Dodoma.
Aliongeza kuwa China na Tanzania
ni marafiki wa muda mrefu na mataifa hayo yanashirikiana vizuri katika
ujenzi wa miundombinu mbalimbali hivyo Serikali inatarajia mengi kutoka
kwenye kampuni hiyo kupitia kwa mwenyekiti wake Bw. Meng.
“Dodoma kuna fursa za uwekezaji
kwenye sekta nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda. Mnaweza
kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za makazi, ofisi, huduma za kijamii na
viwanda ,”
Kwa upande wake Bw. Meng amesema
kampuni yake itaungana na Serikali katika kuboresha Makao Makuu ya
Serikali na inatarajia kutuma wataalam wake mkoani Dodoma kuangalia
maeneo ya uwekezaji.
‘Nataraji tutakuwekeza katika
ujenzi wa miundombinu, nyumba za makazi, ofisi, maeneo ya kutolea huduma
za jamii na teknolojia zitakazowezesha upatikanaji wa maji safi na
salama.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
- L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, OKTOBA 10, 2016


No comments:
Post a Comment