
Waziri wa Mambo ya Katiba na
Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe, amempongeza Balozi Vo Than Nam wa
Vietnam anayemaliza kipindi chake nchini, kwa mchango wake mkubwa katika
kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi kati ya Vietnam na
Tanzania.
Dkt Mwakyembe alitoa pongezi hizo kwenye hafla ya
kuadhimisha miaka 71 ya uhuru wa Vietnam iliyofanyika katika Hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam jana jioni.
Dkt Mwakyembe alisema uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni
ya Vietnam ya Halotel katika sekta ya mawasiliano ni moja ya mafanikio
makubwa ya mahusiano ya nchi mbili hizi.Amesema milango iko wazi kwa makampuni zaidi kutoka Vietnam kuwekeza chini katika sekta mbalimbali na kuongeza kuwa uzoefu ambao Vietnam imeupata katika mageuzi yake ya uchumi kutoka uchumi wa kilimo hadi wa viwanda ni chachu kwa Tanzania inayofuata njia hiyohiyo.
Akimkaribisha Waziri huyo aliyekuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo, Balozi Vo Than Man aliwasifu Watanzania kwa moyo wa ushirikiano na kuahidi kuendeleza mahusiano kati ya nchi hizo


No comments:
Post a Comment