Meneja
wa Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo, akizunguza kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo
katika Shule ya Saint Mary’s Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
Siku
ya Posta duniani huadhimishwa ifikapo Oktoba 09 kila Mwaka ikiwa ni
sehemu ya kumbukumbu ya Siku ya kuanzishwa kwa Umoja wa Posta Duniani
ulioanzishwa mwaka 1874 katika mji wa Berne nchini Switzerland
ukijumuisha mataifa 192 duniani.
Na BMG
Maadhimisho
hayo yamekwenda sambamba na zoezi la kukabidhi zawadi kwa Washindi wa
Uandishi wa barua Kitaifa kutoka mkoani Mwanza ambapo washindi watano
kati ya 10 bora kitaifa wametoka Saint Mary’s Seminary (Nyegezi
Sekondari) Jijini Mwanza.
Washindi
hao na nambari walizoshika kwenye mabano ni, Denis Bahati Stephen (01),
Samwel Lufungulo Somelo (02), Vitalis Aloo Awasi (03), Kizito Eliakimu
Paschal (04) na Fredrick Elias Mayunga (08).
Washindi
wa Tano na Sita wametoka Shule ya Mazinde Juu mkoani Tanga, Mshindi wa
Saba ametoka Shule ya Lugalo mkoani Iringa, huku Washindi wa Tisa na 10
pia wakitoka Shule ya Mazinde Juu mkoani Tanga.
Meneja
wa Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo amesema shindano la uandishi wa
barua huwashirikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari
wasiozidi umri wa miaka 15 ambapo shule za msingi lugha ya kiswahili na
kiingereza hutumika na kiingereza pekee kwa shule za sekondari.
Amebainisha
kwamba wanafunzi huandika barua yenye mane kati ya 500 na 1,000
kulingana na mada iliyotolewa na kwamba mwaka huu mada ilikuwa ni
“Jiandikie barua ukiwa na miaka 45” ambapo barua ya mshindi wa kwanza
itakwenda kushindanishwa na barua za washindi wengine kutoka nchi 191
wanachama wa Umoja wa Posta Duniani ambapo mshindi wa kwanza nchini
ataliwakilisha taifa kwenye shindalo hilo nchini Switzerland.
Katibu
Mtendaji wa Idara ya Elimu, Jimbo Kuu la Mwanza, Alex Masasi, ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo akizungumza ambapo
amewahimiza wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao hususani kuwa
bora kwenye kusoma, kuandika na kuzungumza lugha nyingi tofauti na
kiswahili na kiingereza.
Wanafunzi
wakimsikiliza kwa umakini Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu, Jimbo Kuu
la Mwanza, Alex Masasi, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho
Siku ya Posta yaliyofanyika leo Jijini Mwanza


No comments:
Post a Comment