Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ameagiza Jeshi la Polisi mkoani
Mbeya kuwakamata walimu walioonekana kwenye video wakimwadhibu
mwanafunzi vibaya. Tukio hilo lilitokea 28. September.
Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo.
Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian , darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndipo walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga .
Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza na ndiye aliyechukua video.
Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya



No comments:
Post a Comment