MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umepokea ugeni kutoka Wizara ya Afya ya
Zanzibar katika ziara ya mafunzo iliyoongozwa na Mh.Mahamud Thabit
Kombo ambaye ni Waziri wa Afya wa Zanzibar.
Katika ziara hiyo yenye lengo
la kushiriki uzoefu wa utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo, Waziri na
timu yake walipata melezo na kujionea shughuli mbalimbali za Mfuko huo.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mh.Kombo alisema “tunahitaji kujifunza kutokana na uzoefu wenu wa kuendasha Mfuko wa bima ya afya, hatukuona haja ya kwenda mbali kwani tuna kaka na dada zetu hapa karibu na wana uzoefu wa kutosha”.
Mh. Kombo alisema kuwa Wizara ya Afya ya Zanzibar ina ushirikiano mkubwa sana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na  kusisitiza kuwa Wizara hizi zinafanya kazi kwa karibu sana na hii inasaidia kufanikisha maendeleo ya sekta ya afya kwa pande zote.
Akiwakilisha mada ya Utekelezaji wa shughuli za Mfuko,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga aliongelea umuhimu wa Bima ya Afya katika maendelea ya sekta ya afya nchini na kuanisha utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo ambapo alielezea pia mifumo imara ya uendeshaji wa Mfuko ikiwemo ya Tehama lakini pia mifumo  ya kubaini udanganyifu ili kuudhibiti.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) lielezea umuhimu wa Mfuko kujipanga kimuuondo katika kuhakikisha unaweza kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha afya bora kwa wote. “Pamoja na mambo mengine, elimu kwa umma ni suala la msingi sana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko na kuwapa nafasi wadau kuuliza na kujibiwa hoja zao”alisema.
Akitoa shukrani zake kwa NHIF katika ziara hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari, Waziri Kombo alishukuru Mfuko na kusema kwamba utabakia kwenye historia ya maendeleo ya sekta ya afya Zanzibar lakini pia alisisitiza umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwa kusema “Bima ya afya ni Mkombozi wa wanyonge”.
![]() |
| Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo akizungumza na viongozi mbalimbali wa NHIF kuhusu kujifunza kutokana na uzoefu  wa kuendesha Mfuko wa bima ya afya, katika ziara ya mafunzo makao makuu ya NHIF leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu). |



No comments:
Post a Comment