Taasisi
ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyo chini ya Wizara ya
Fedha,(UTT-PID) imetoa kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kwa ajili ya
kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba Mkoani Kagera
hivi karibuni.
Tukio
hilo la kukabidhi fedha hizo zilizowakilishwa kwa njia ya mfano wa
hundi limefanyika leo Oktoba 7.2016, katika ofisi za Msajili wa Hazina
Jijini Dar es Salaam kwa Msajili wa Hazina.
Awali
akipokea ujumbe uliomwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo ya
UTT-PID, Msajili wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru ameshukuru UTT-PID kwa
wito wao huo wa kuchangia maafa kwa kuwakumbuka wananchi hao ambao wengi
wao wanahitaji msaada mkubwa.
Naye
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa UTT –PID, Ndugu Uli Mtebe alimweleza
Msajili huyo wa Hazina kuwa, Taasisi yao imekuwa karibu na watu wa
Kagera-Bukoba kwani licha ya kufanya miradi, pia wamekuwa karibu na
jamii hiyo kwa kuwachangia mambo ya kimaendeleo ikiwemo elimu na
miundombinu.
Msajili wa Hazina Ndugu Lawrence
Mafuru akipokea mfano wa Hundi kutoka kwa wakilishi wa Mkurugenzi Mkuu
wa UTT – Projects Ndugu Uli Mtebe na Afisa Masoko wa UTT Projects Bi.
Kilave Atenaka kiasi cha shilingi milioni kumi kwa niaba ya Kamati ya
Maafa Bukoba chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.
Msajili wa Hazina Ndugu Lawrence
Mafuru akipokea mfano wa Hundi kutoka kwa mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu
wa UTT – Projects Ndugu Uli Mtebe kiasi cha shilingi milioni kumi kwa
niaba ya Kamati ya Maafa Bukoba chini ya ofisi ya Waziri Mkuu. Kulia ni
Afisa Masoko wa UTT Projects Bi. Kilave Atenaka.
Msajili wa Hazina Ndugu Lawrence
Mafuru (katikati) akimsikiliza mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa UTT
–PID, Ndugu Uli Mtebe wakati akielezea shughuli za Taasisi hiyo






No comments:
Post a Comment