KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 1, 2016

YANGA SIMBA HAKUNA MBABE

0001
Mchezaji wa timu ya Yanga Thaban Kamusoko akikokota mpira mbele ya Ibrahim Ajib mchezaji wa timu ya Simba pia ya jijini Dar es salaam  wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam timu hizo zikitoshana nguvu kwa kufungana magoli 1-1 huku timu ya simba ikicheza pungufu kwa muda mrefu baada ya mchezaji wake Jonas Mkude kutolewa kwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo.
Goli la timu ya Yanga limefungwa na mchezaji Hamisi Tambwe katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo huku timu ya Simba ikisawazisha kwa mpira wa kona katika kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji wake Shiza Kichuya ambaye alipiga kona na kujaa wavuni moja kwa moja huku akiacha mshangao kwa wachezaji wa Yanga ambao walikuwa tayari wamekaa golini ili kuodoa mpira huo bila mafanikio.
1
Timu za Simba na Yanga zikiingia uwanjani kabla ya mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
2
Wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakisalimiana kabla ya mchezo huo.
3
Kikosi cha Simba kikiwa katika picha ya pamoja.
4
Kikosi cha Timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment