KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 26, 2016

YANGA YANG’ARA BILA PLUIJM YAICHAKAZA JKT RUVU4-0, CHIRWA AENDELEA KUTISHA

Na.Alex Mathias,Dar es salaam.

index

Timu ya Yanga imeshuka bila ya Kocha Pluijm,aliyeachia ngazi kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam wakiwa chini ya Mwambusi vijana wa jangwani wameng’ara zaidi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu na kufanya timu hiyo kuwa na mabao 10 kwa michezo miwili ikumbukwe walimfumua Kagera 6-2.

Yanga waliandika goli la mapema dakika ya 6 likifungwa na mshambuliaji Obrey Chirwa baada ya makosa ya walinzi wa Ruvu kujichanganya na kumkuta mfungaji akiwa katika nafasi nzuri ya kuiandikia goli huku likiwa goli la tano kwa Chirwa ambaye ameendelea kung’ara kila mechi.

Baada ya kufungwa goli hilo timu zote ziliendelea kupata nafasi nyingi za wazi na kushindwa kupata magoli mengi zaidi huku kiungo cha kati cha wanajeshi hao kikipotea kabisa hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele.

Kipindi cha pili kilianza kwa wenyeji Yanga kukosa nafasi za wazi kupitia kwa Donaldo Ngoma pamoja na Msuva baada ya kuona hivyo Kocha Mwambusi alimtoa Ngoma dakika ya 54 na nafasi yake kuchukuliwa na Amis Tambwe.

Dakika ya 63 Tambwe aliiandikia Yanga goli la pili na likiwa la tano kwake baada ya kuichambua ngome ya Ruvu na kuwafanya wapotezee zaidi na kukubali kuendelea kushambuliwa kama nyuki Simon Msuva alifunga la tatu mnamo dakika ya 82 naye likiwa la tano msimu huu wa Ligi.

Tambwe alifunga la nne dakika za majeruhi likiwa la sita kwake msimu huu na kuendelea kumfukuzia Shiva Kichuya mwenye magoli 7 hadi mpira unamalizika Yanga wameibuka na ushindi wa magoli 3-0 wakiwa chini ya kocha Mwambusi kwa matokeo hayo mabingwa hao wamefikisha pointi 24 kwa mechi 11 kwenye Ligi kuu wakiwa wanazidiwa alama 5 na Simba ambao wana pointi 29 ila wote wakiwa wamecheza jumla ya mechi 11.

No comments:

Post a Comment