KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 26, 2016

YANGA YASEMA NI UZUSHI BADO HATUJAINGIA MKATABA NA LWANDAMINA TOKA ZAMBIA,TUNA IMANI NA MWAMBUSI.

index

Na.Alex Mathias,Dar es salaam.

Timu ya Yanga imekanusha taarifa zinazozagaa kwenye mitandao kuwa wameingia mkataba na kocha kutoka Zambia kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Hans Van Der Pluijm aliyetangaza kujiuzulu kutokana na kukerwa na baadhi ya matamshi ya uongozi huo.

Akizungumza na FULLSHANGWEBLOG.COM,Kaimu katiba Mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedit,amesema kuwa mpaka sasa kuna majina matano ya makocha ambao wameleta CV zao kwa ajili ya kuomba kuifundisha Yanga hivyo mashabiki watulie kipindi hiki na kuacha kusikiliza maneno ya watu kwani bado hatujaingia mkataba na George Lwandamina.

“Tunaomba watu watuelewe kuwa sisi bado hatujaingia mkataba wowote na kocha huyu ila hata yeye tayari kaleta CV yake na kamati yaa utendaji itakaa na kupitia majina hayo na itatangaza na pia watu wajue kuwa George Lwandamina bado ana mktaba na timu yake ya Zesco United na unatarajia kumalizika mwakani,”alisema Deusdedit

Aidha amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuwa wasiwe na wasiwasi muda sio mrefu kamati ya usajili itakaa kwa pamoja na kupitia hayo majina hivyo wataweza kutangaza jina la huyu kocha atakayepita kuchukua mikoba ya Hans Van Der Pluijm.

iIla kwa sasa timu ipo chini ya Kocha Msaidizi Juma Mwambusi na kesho anatarajia kuiongoza itakapocheza kiporo chake dhidi ya wanajeshi JKT Ruvu katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Kwa upande wa Pluijm leo alitinga mazoezini na kuwaaga wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi na kutoa wosia kidogo kwa wachezaji na kuwataka wapambane ili wawezi kutetea ubingwa msimu huu na kuendelea kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa benchi jipya litakalotangazwa.

No comments:

Post a Comment