Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi
Serikalini (GPSA) Jacob Kibona akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo
pichani) faili lenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye
mamlaka ya kusambaza mafaili hayo kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya
serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.
|
Na Barnabas Lugwisha
Serikali kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini
(GPSA) hivi karibuni imeokoa shilling bilioni 1.3 baada ya wakala hiyo kununua kwa
pamoja magari 392 katika mpango wa serikali wa manunuzi ya pamoja.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw Jacob Kibona, amewaambia
Waandishi wa Habari jana kuwa fedha hizo zimeokolewa na serikali baada ya kununua
magari 392 kwa pamoja kwa Sh. bilioni 56.1 badala ya shilingibilioni 58.1 iwapo
kila taasisi ingenunua magari yake.
“Kwa kweli huu mpango wa manunuzi yapamoja ni mpango mzuri sana
ambao unaiwezesha serikali kuokoa fedha nyingi,” Alisema
Alisema fedha zilizookolewa zitaiwezesha serikali kufanya shughuli
nyingine za maendeleo ya ummana kama vile kuboresha miundombinu ya barabara,
huduma za afya na elimu.
Amesema taasisi yake pia katika kipindi cha Julai hadi Oktobamwaka
huu, imezikabidhi taasisi za serikali magari
ya aina mbalimbali yapatayo 136.
Alisema katika kuhakisha kwamba wanapunguza gharama katika manunuzi,
wamekuwa wakinunua bidhaa kutoka kwa wazalishaji moja kwa moja ila inaposhindikana
kutokana na sera za makampuni makubwa kuwa na mawakala wa usambazaji wamekuwa wakinunua
kwa mawakala hao kwa makubaliano maalum ya kupunguza bei.
Alisema kuwa kazi nyingine muhimu ya taasisi yake ni kugomboa
mizigo kupitia bandarini , viwanja vya ndege na mipakani kwa niaba ya serikali ambapo
kwa mwaka wa fedha uliopita waligomboa mizigo yenye thamani ya Shlingi bilioni
62.7.
Alisema mizigo hiyo ilikuwa ni pamoja na vifaa vya mkongo wa
taifa, vifaa vya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wizara yaMali asili na utalii.
Aliongeza kuwa kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu pia walikomboa vifaa mbalimbali vya serikali
zikiwamo ndege mbili zilizonunuliwa na serikali kutoka Canada aina ya Bombadier
vyote vikiwa na thamani ya Shilingi bilioni 100.97.
Alisema GPSA ina huduma za kuhifadhi vifaa kwa ajili ya taasisi
za serikali, kwa kuwa wao wana maghala makubwa katika mikoa karibu yote .
“Hata mkoani Kagera baada ya maafa ya tetemeko la ardhi,
maghala yetu yanayotumika kuhifadhi vifaa mbalimbali viliyotolewa kama misaada,”
Pia wana jukumu la kutoa huduma ya mafuta kwa magari yaserikali na kwamba kwamba
hadi sasa wamefanikiwa kusimika mfumo wa usimamizi wa mafuta kwa matumizi ya ya serikali na kwamba mfumo huo unaendelea kupanuliwa
ili uzifikie taasisi nyingi za umma.
Alizishauri taasisi za umma kuzingatia sheria za
manunuzi kwa lengo la kutoa huduma bora na kwa kuhakikisha kuwa vifaa na huduma
zinazopatikana zinazingatia thamani halisi ya fedha zinazotumika
No comments:
Post a Comment