![]() |
Kikosi cha Azam FC
kinachojiandaa kupambana na Yanga Jumamosi ijayo katika mchezo wa Ligi
Kuu Bara, kimeingiwa na hofu juu ya mchezo huo baada ya kocha wake
msaidizi, Idd Nassor Cheche kusema katika maandalizi yao kuna vitu
wanavikosa.
Aprili Mosi, mwaka
huu katika Uwanja wa Taifa, Dar, Yanga na Azam zinatarajiwa kupambana
kuelekea michezo ya mwisho ya kuhitimisha msimu huu ambapo mara ya
mwisho timu hizo kukutana kwenye ligi zilitoka suluhu.
Azam ambayo inashika
nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 44,
imekuwa ikijiandaa kupambana na Yanga huku ikiwakosa nyota wake saba
waliopo katika kikosi cha Taifa Stars ambao ni Aishi Manula, Shomari
Kapombe, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Frank Domayo, Salum Abubakar na
Himid Mao.
Cheche amesema:
“Siku zote maandalizi ya pamoja ndiyo mazuri lakini inapotokea wachezaji
wengi wamekosekana lazima kunakuwa na athari.
“Kwa sasa tunatafuta
namna ya kufanya ili kukabiliana na hali hiyo kwa sababu ukiachana na
siku hizi chache ambazo wengine hawapo, hapo nyuma walikuwa pamoja,
hivyo kilichobaki tuombe Mungu huko walipo wasipate majeraha ili siku ya
mchezo wetu dhidi ya Yanga wawepo wote.
“Tunajua kwamba
mchezo utakuwa mgumu, lakini tunaamini kadiri siku zinavyokwenda tutajua
uwezo wetu wa kupambana nao umefikia wapi ila kwa sasa tunafahamu
kwamba mchezo utakuwa mgumu kutokana na kwamba kuna timu zinasaka
ubingwa na nyingine zikitafuta kulinda heshima.”
|
March 27, 2017
AZAM FC YAINGIWA NA HOFU DHIDI YA YANGA VPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment