![]() |
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es salaam wakati alipokuwa akitangaza mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka
linalotarajiwa kufanyika Aprili 16 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam. Msama amemtaja Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mwigulu
Nchemba kuwa ndiye atakuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
Ameongeza kuwa maandalizi ya
tamasha hilo yanaendelea vizuri na karibu mambo mengi yako tayari kwa
ajili ya tamasha hilo litakalofanyika pia katika mikoa kadhaa, Ambayo ni
Simiyu, Dodoma Iringa, Mwanza na Geita.
|
![]() |
| Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa Break Point Kinondoni jijini Dar es salaam. |




No comments:
Post a Comment