![]() |
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) imekanusha juu ya uvumi
unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uuzaji wa viwanja katika
eneo ka Mkonze lililopo mkoani Dodoma.
Tamko hilo limetolewa hivi
karibuni mkoani Dodoma na Kaimu Meneja Uhusiano wa CDA, Angela Msimbira
kutokana na kusambaa kwa ujumbe huo katika mitandao mbalimbali ya
kijamii.
Bi. Angela amesema taarifa hizo
ambazo hazieleweki zimekuwa zikidai kuwa viwanja hivyo ni halali na
ukinunua unapewa hati na CDA ambayo ndiyo imepewa dhamana ya ugawaji wa
viwanja mkoani humo.
“Mamlaka yetu inapenda kuutarifu
Umma kuwa taarifa hizo si za kweli hivyo wananchi wanatakiwa kuzipuuza
na kuendelea kufata utaratibu kwani mamlaka hiyo ina utaratibu
uliopangwa wa namna ya kupata viwanja vilivyo halali,”alisema Bi.
Angela.
Amefafanua kuwa Mamlaka hiyo
inapotaka kuuza viwanja hutumia utaratibu wa kutangaza kwenye vyombo vya
habari, mitandao ya kijamii pamoja na kutoa matangazo kwa umma kwa njia
ya vipaza sauti.
Aidha, Bi. Angela ametumia fursa hiyo kuendelea kuwakumbusha wananchi kufuata taratibu za upatikanaji wa viwanja.
Kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha
Sheria ya Makosa ya Jinai Mitandaoni ya mwaka 2015, ni kosa kwa mtu
yoyote kutangaza, kuchapisha au kueneza habari za uongo au uzushi katika
mitandao.
|
March 8, 2017
CDA YAKANUSHA UUZAJI WA VIWANJA MKONZE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment