![]() |
Nahodha
wa Manchester United Wayne Rooney hataweza kuchezea klabu hiyo wakati
wa mechi ya robo fainali Kombe la FA dhidi ya Chelsea uwanjani Stamford
Bridge Leo Mechi hiyo itachezwa saa tano kasorobo saa za Afrika
Mashariki.
Rooney aligongana na Phil Jones wakifanya mazoezi na akaumia mguuni.
Mshambuliaji mwingine wa United
Zlatan Ibrahimovic atakuwa anaanza kutumikia marufuku ya kutocheza mechi
tatu, adhabu aliyopewa kwa kumgonga Tyrone Mings wa Bournemouth kwa
kiwiko cha mkono.
Washambuliaji wengine wa United Anthony Martial na Marcus Rashford wanaugua na hawataweza kuchezea mashetani hao wekundu.
Kikosi cha Antonio Conte kiko shwari bila wachezaji wowote kutatizwa na majeraha au kupigwa marufuku.
Conte amesema ni wazi kwamba
Manchester United na Manchester City ndio wenye vikosi vya wachezaji
stadi zaidi Ligi Kuu ya Uingerez na hivyo basi anatarajia upinzani
mkali.
“Ningependa kuangazia zaidi mechi na wachezaji wangu,” amesema.
Meneja wa United Jose Mourinho,
ambaye wachezaji wake walisafiri Urusi kwa mechi ya Ligi ndogo ya klabu
Ulaya, Europa League, Alhamisi wiki iliyopita, amesema Manchester United
hawababaishwi na Chelsea licha ya wasiwasi kwamba huenda wachezaji wake
wakatatizwa na uchovu.
“Manchester United ni klabu kubwa. Manchester United ndiye bingwa wa michuano hii.
“Si makosa ya Chelsea kwamba
tulipangiwa kucheza mechi hii Jumatatu, kwa hivyo ni wazi kwamba
tutafanyia kikosi chetu mabadiliko … lakini hatuwezi kwenda Stamford
Bridge na timu ya Nicky Butt (wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23).
Ni mara ya 12 kwa United na
Chelsea kukutana Kombe la FA. Katika mechi 11 za awali, United
wameshinda mechi nane na Chelsea tatu.
Blues hata hivyo walishinda mechi
zote mbili zilizokutanisha timu hiyo mbili Kombe la FA mwongo huu,
wakishinda 1-0 fainali 2007 na pia raundi ya sita uwanjani Stamford
Bridge mwaka 2013 walipoibuka na ushindi wa 1-0.
Chelsea hawajashindwa mechi 11
walizocheza karibuni ligini na katika vikombe dhidi ya United
(wameshinda sita na kutoka sare tano), na wamefungwa mara tatu pekee
katika mechi tisa za karibuni zaidi.
|
March 13, 2017
MAN UNITED BILA IBRAHIMOVIC NA ROONEY KUWAVAA CHELSEA KOMBE LA FA LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment