![]() |
Ikulu,Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Machi 2017, amekutana na
kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu ya Chamwino mjini
Dodoma.
Dkt. Magufuli amesema katika
mazungumzo yao wamezungumza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtakia
heri Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali
Mohamed Shein kufuatia leo kuwa siku yake ya kuzaliwa.
Kwa upande wake Rais Dkt. Ali
Mohamed Shein amesema anamshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa kumtakia heri
katika siku yake muhimu ya kuzaliwa na hivyo wamekutana kubadilishana
mawazo katika kuhakikisha wanajenga nchi na kusonga mbele.
”Siku ya kuzaliwa ni siku ya
furaha lazima ikumbukwe lazima isherehekewe, mimi siku yangu ya kuzaliwa
sisherehekei sana lakini huwa nafurahi sana na leo nimefurahi sana” amesema Dkt. Shein.
Dkt.Shein amesema ametumia siku
yake ya kuzaliwa kumtembelea Rais Dkt.Magufuli ili waweze kubadulishana
mawazo kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
13 Machi, 2017
|
March 13, 2017
RAIS DKT.MAGUFULI AKUTANA NA RAIS DKT.SHEIN IKULU DODOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment