![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness William Seneda (katikati), akihutubia kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani Kisarawe jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga’alo. |
| Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile, akipima shinikizo la damu katika maadhimisho hayo. |
| Ofisa Mikopo wa Benki ya Equity, Nelifyage Mbwilo (kulia), akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (wa pili kushoto), wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya wajasiriamali katika maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga’alo na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile. |
| Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Wilaya ya Kisarawe wakionesha kazi wazifanyazo. |
| Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneka (katikati kulia na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga’alo wakiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Skauti wakati wa maadhimisho hayo. |
| Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Ntela Mwampamba (kushoto), akizungumza kwenye maadhimisho hayo. |
| Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga’alo, akihutubia kwenye hafla hiyo. |
| Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Seneda akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 61,550 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wilayani humo iliyotolewa na Benki ya NMB. |
| Wadau wa maendelea wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya hiyo baada ya kukabidhi msaada wa magodoro na vifaa vingine vyenye thamani ya sh.700,000. |
| Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Kwanza Foundation, Hidaya Chomvi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya baada ya kumkabidhi zawadi. |
Brass Bandi ya Magereza ikitumbuiza kwenye maadhimisho hayo.
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa
Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameziagiza Halmshauri zote za
mkoa huo kuhakikisha kuwa zinatenga asilimia tano ya mapato yao ya ndani
kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake.
Agizo
hilo lilitolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness
Seneda kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani humo
jana. Ndikilo alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.
“Wakurugenzi
wa Halmashauri ambazo hazitatekeleza wajibu wahakikishe wanajitahidi
kufanya jukumu hilo muhimu kwa maendeleo ya wanawake wa mkoa huo”
alisema Seneda.
Alisema
katika kuwawezesha wanawake kiuchumi, Serikali imeanzisha Benki ya
Wanawake Tanzania, mifuko mbalimbali ukiwemo mfuko wa maendeleo ya
wanawake (WDF) pamoja na kuhamasisha uanzishaji wa Saccos, vikundi vya
uzalishaji mali na Vicoba na kwa kupitia fursa zilizopo kuwawezesha
wanawake wajasiriamali kupata mikopo yenye masharti nafuu.
Alisema
katika mkoa huo kuna jumla ya vikundi vya uzalishaji mali 1, 350 vyenye
wanachama 5,411 lengo likiwa ni kumuwezesha mwanamke kushiriki katika
kuleta mabadiliko ya kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa
ujumla.
Seneda
akizungumzia wilaya yake alihimiza suala zima la elimu na kuwataka
wazazi kuwa mstari wa mbele kusimamia watoto wao na kupiga vita mimba za
utotoni na kuwaoza watoto wao.
Alisema serikali haitamvumilia mzazi au mlezi yeyote atakayebainika kuozesha mtoto wake na mtu atakaye mpa mimba mwanafunzi.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) |



No comments:
Post a Comment