![]() |
Na.Alex Mathias
Timu ya Zanaco FC toka Zambia
ambao ni wapinzani wa Yanga katika Michuano ya Klabu bingwa barani
Afrika wanatarajia kuwasili leo kwenye ardhi ya Tanzania Majira ya saa
kumi jioni kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa Shirika
la Ndege la Rwanda.
Zanaco FC ambao Jumamosi ya wiki
hii watashuka dimbani kucheza na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya
Tanzania bara Yanga katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwania
nafasi ya kutinga hatua ya Makundi.
Mabingwa watetezi hao wa Zambia
hii itakuwa mara ya pili kukutana na Yanga katika mashindano ya CAF
kwani walikuja mwaka 2006 ambapo waliweza kuwang’oa Yanga kwa jumla ya
magoli 3-2,Mchezo wa kwanza ulichezwa Dar es salaam na Yanga kuibuka na
ushindi wa magoli 2-1 na ilipoenda enda Zambia Yanga walifungwa 2-0 na
Zanaco kusonga mbele kwa jumla ya magoli 3-2.
Yanga itaingia uwanjani kwa lengo
la kulipa kisasi huku ikiwa na morali ya kuwa na kocha Mzambia ambaye
anaifahamu vyema Zanaco kwani Msimu uliopita alikuwa anakinoa kikosi cha
Zesco United ambao walifika nusu Fainali ya Michuano klabu bingwa
Afrika.
Zanaco FC wamekuwa wasili kusema
kuwa watawasili lini ila uchunguzi uliofanywa na mtandao wa
FULLSHANGWEBLOG kuwa timu hiyo itawasili Leo majira ya saa kumi na
dakika tano tayari kwa mtanange huo wa Jumamosi.
|
March 9, 2017
WAPINZANI WA YANGA CAF KUTUA LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment