![]() |
Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys,
jana walikabidhiwa Kadi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Shirika
Bima la Afya la Taifa (NHIF) kwa lengo la kuwasaidia kupata matibabu ya
uhakika wanapokuwa wanaumwa.
Timu hiyo kwa sasa inajiandaa na michuano ya mataifa Afrika kwa vijana inayotarajia kufanyika nchini Gabon, Mei, mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi wa
Masoko na Utafiti wa NHIF, Angela Mziray amesema kuwa lengo la kutoa
kadi hizo kwa wachezaji hao ni kuwasaidia kupata matibabu kwa urahisi
katika vituo vyote nchini hata wakiwa nje ya majukumu ya timu ya taifa.
“Kadi za Bima ya Afya
ni zinatoa mfumo rahisi wa kuweza kupata matibabu na lengo la kufanya
hivi ni kuweza kuwasaidia vijana hawa ambao ni matarajio ya kesho kwani
hii siyo mara ya kwanza kufanya kazi na Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) na sasa hivi tunatoa huduma katika vituo 6,500 nchini.
“Kiukweli hili siyo
jambo dogo kwa vijana wetu maana linaleta hamasa na umuhimu mkubwa
kutokana wao kuweza kuwa na uhakika wa kupata huduma bora za Afya kwa
kadi ambazo tunawapatia kwa sababu wao wanafanya mazoezi na wanaweza
wakaumia hivyo zitawasaidia katika kupata huduma nzuri bila ya kutumia
pesa yoyote kutoka mkononi mwao,” alisema Mziray.
Upande wa Katibu Mkuu
wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema wanashukuru mfuko huo kutokana na
mchango huo waliutoa kwa timu huyo huku akiwaomba wawe sehemu ya
wadhamini wa timu hiyo inayojiandaa na fainali za Afrika nchini.
|
March 24, 2017
SERENGETI BOYS WALIVYOLAMBA BIMA YA AFYA KUTOKA NHIF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment