![]() |
Benjamin Sawe,Dar es Salaam
Serikali kupitia Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema mpaka kufikia mwaka 2020
litawawezesha watanzania kutumia gesi majumbani mwao hivyo kupelekea
upungufu wa uharibifu wa mazingira nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Eng.
Kapuulya Musomba amesema muda mrefu kumekuwa na uharibifu wa mazingira
hivyo kupatikana kwa nishati ya mafuta na gesi kutaiwezesha Tanzania
kuwa mahali salama kimazingira ikiwa ni pamoja na ukuaji wa sekta ya
uchumi.
Alisema katika robo ya pili ya
mwaka 2017 shirika limekamilisha usambazaji wa mabomba ya gesi kwa
matumizi ya majumbani jijini Dar es Salaam na zaidi ya viwanda 300
vimeunganishwa na nishati ya gesi hapa nchini hivyo kupelekea
upatikanaji wa umeme wa uhakika.
Kuhusu upangaji wa Bei kwa
matumizi ya gesi itakayosambazwa majumbani Eng. Musomba amesema Taasisi
yake itashirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Hivi sasa zaidi ya asilimia 50 ya
umeme uliopo katika Gridi ya Taifa unatokana na gesi asilia hivyo
mipango ya Serikali ni kulifanya Shirika hilo kuchangia zaidi mapato
Serikalini yanayotokana na rasilimali hiyo.Alisema Eng. Musomba
Alisema TPDC imejipanga kuwekeza
kwenye shughuli za utafutaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa
gesi ili Taifa linufaike na rasilimali hiyo.
Akitolea mfano mradi mkubwa wa
kusindika gesi asilia (Liqufied Natural Gas-LNG), Eng. Musomba
alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya mzigo wa
kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa mauzo.
Alisema kukamilika kwa mradi wa
(Liqufied Naturla Gas- LNG)utakuwa ni fursa kwa watanzania kupata ajira
katika mradi huo ikiwa ni pamoja na kuchangia pato la
mwananchi,wawekezaji na Taifa kwa ujumla.
Alisema uwekezaji katika sekta
ya mafuta na gesi ni wa gharama kubwa na hata mafaniko kwa maana ya
mapato makubwa kwa Serikali huchukua muda mrefu kuonekana hivyo
amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kuilinda miundombinu inayopita
maeneo yao.
TPDC inaendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuongeza uelewa zaidi katika sekta hiyo ya gesi na mafuta.
|
March 24, 2017
WATANZANIA KUNUFAIKA NA GESI ASILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment