KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 8, 2017

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, WAZIRI KAIRUKI AONGOZA KUFANYA USAFI MUHIMBILI

 Waziri Kairuki (wa pili kutoka kushoto) akifanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uuguzi wa Muhimbili, Agness
Mtawa. Kutoka kulia wa kwanza ni Katibu wa Umoja wa Wanawake katika Wilaya ya Ilala, Joyce Ibrahimu Mkaugala na Zuhura Mawona wakifanya usafi Leo katika hospitali hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki akizungumza na wafanyakazi
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo kabla ya kukabidhi vitanda 10 na
magodoro 10 kwa uongozi wa hospitali hiyo. Katika kusherekea siku ya wanawake
duniani leo, pia Waziri huyo amewapatia kinamama zawadi mbalimbali zikiwamo
nguo za watoto na sabuni. Kushuto Mkurugenzi wa Uunguzi katika hospitali hiyo,
Agness Mtawa.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki akikabidhi  vitanda 10 na magodoro 10 kwa Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Agness Mtawa.
 Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akimshukuru Waziri Kairuki baada ya kupokea msaada wa vitanda na magodoro leo.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Hospitali ya Taifa Muhimbili –MNH- leo imeungana na wanawake
wengine ulimwenguni kote kuadhimisha siku ya wanawake Duniani kwa kufanya usafi
katika maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
 
Zoezi hilo limeongozwa na Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Dar
es salaam Mheshimiwa Angellah Kairuki kwa niaba ya Umoja wa Wanawake wa Chama
cha Mapinduzi –UWT- mkoani humo.
 
Mheshimiwa Kairuki ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi na Utawala Bora amesema katika kusheherekea siku ya wanawake
Duniani UWT  imeona ni vema wakashiriki
katika shughuli mbalimbali za kijamii ili kuonesha dhamira ya dhati kwamba CCM
inawajali wananchi wake bila kujali itikadi ya chama.
 
‘’ Sisi tumekuja hapa Muhimbili kushiriki na nyinyi katika kuadhimisha
siku hii kwa kufanya usafi bila kujali itikadi ya chama kwani Hospitali hii
inahudumiwa wananchi wote , pia  siku hii
ya leo tunatoa msaada wa vifaa mbalimbali vya watoto na  wenzetu wengine wameenda katika Hospitali
zingine wote tukiwa na lengo moja’’. Amesema Waziri Kairuki.
 
‘’Msaada tuliotoa ni  vitanda kumi, magodoro kumi , mashuka  na vifaa vingine mbalimbali vya watoto
zikiwamo nguo ,sabuni na Pampers  lengo
ni kuunga mkono juhudu za serikali za kuboresha huduma za afya hususani  afya ya mama na mtoto na kuhakikisha hakuna
mgonjwa anayelala chini kwa kukosa kitanda’’ . Amesema Mheshimiwa Kairuki.
 
Akipokea msaada wa vitanda hivyo Mkurugenzi wa Huduma za
Uuguzi na Ukunga wa MNH  Agnes  Mtawa amewashukuru UWT kwa msaada walioutoa
ambao amesema umekuja wakati muafaka kwani utasaidia katika kutekeleza majukumu
yao .
 
Hata hivyo Mkurugenzi Mtawa amewakumbusha wauguzi kuendelea
kufanya kazi kwa kufuata maadili na kusisitiza kuwa kazi hiyo inahitaji kujitoa
na kuwa na moyo wa huruma .
 
Siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila Machi nane ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’ Tanzania ya Viwanda , Wanawake ndio msingi wa
mabadiliko ya kiuchumi .

No comments:

Post a Comment