![]() |
| Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Bi devota Mdachi akizungumza na Mabalozi waliomtembelea ofisini kwake jana.Kushoto ni Balozi Omari Yusuph Mzee na kulia ni Balozi Abdallah Kilima. |
![]() |
| Balozi mteule wa Tanzania nchini Kenya Dkt Pindi Chana akisisitiza jambao wakati wa mazungumzo baina yao na Mkurugenzi Mwendshaji wa TTB walipomtembelea ofisini kwake Dar es salaam. |
![]() |
| Mkurugenzi Mwendshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi (kulia) akimkabidhi Balozi Abdallah Kilima moja ya majarida ya TTB yanayozungumzia utalii wa Tanzania wakati timu ya mabalozi sita walioteuliwa hivi karibuni walipomtembela Mkurugenzi huyo ofisini kwake jijini Dar es salaam. |
![]() |
Mabalozi wanaowakilisha
Tanzania katika baadhi ya nchi duniani wakiwai katika picha ya pamoja na
Mkurugenzi wa TTB Bi Devota Mdachi (wa nne kushoto) na baadhi ya
Maafisa waandamizi wa TTB . Kutoka kushoto ni Bw. Geofrey Meena Meneja
Masoko wa TTB, Mh. Balozi dkt Pindi Chana , Mh. Balozi Omari Yusuph
Mzee, Mh. Balozi Fatma Rajab (wa tano), Mh. Balozi Grace Mgovano (wa
sita), Mh. Balozi Matilda Masuka (wa saba) na Bw. Philip Chitaunga
Meneja Huduma kwa watalii wa TTB.
Na: Geofrey Tengeneza
Mabalozi walioteuliwa hivi
karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani
wameihakikishia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa wamejizatiti
kikamilifu kwenda kusaidia juhudi kubwa za Bodi hiyo katika kuitangaza
Tanzania kama eneo bora la Utalii duniani katika nchi wanazokwenda
kufanyakazi sambamba na kuhamasisha wafanyabiashara kutoka mataifa hayo
kuwekeza nchini katika sekta ya utalii ikiwa ni utekelezaji wa jukumu
lao kubwa la kukuza diplomasia ya uchumi.
Wamepongeza juhudi zinazofanywa na
TTB katika kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii lakini wakaomba
iangalie namna gani inaweza kusaidia katika kuboresha huduma zitolewazo
na wadau wa utalii kwa watalii wanaotembelea Tanzania kama vile
mahotelini kwani bado hatufanyi vema katika suala la huduma bora na
nzuri kwa watalii. Aidha wameiomba TTB kushauri mamlaka na watoa huduma
wengine katika sekta ya utalii kupunguza gharama wanazotozakwani ni
kubwa sana kiasi cha kuifanya Tanzania kulalamikiwa na wageni wengi kuwa
ni eneo la utalii ghali sana ukilinganisha na nchi nyingine ambazo ni
washindani wetu katika sekta ya Utalii.
Hayo yamesemwa leo na mabalozi
hao wakiongozwa na Balozi Omari Yusuph Mzee walipotembelea makao makuu
ya Bodi ya Utalii Tanzania kwa lengo la kuzungumza na Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi hiyo Bi Devota Mdachi na kupanga mikakati ya namna
balozi hizo zinavyoweza kushirikiana na TTB katika kuitangaza Tanzania
na kuhamashisha wawekezaji kutoka nchi wanazokwenda kufanyakazi kuja
nchini kuwekeza katika sekta ya utalii.
Mapema Mkurugenzi Mwendeshaji wa
TTB Bi Devota Mdachi aliwaelezea waheshimiwa mabalozi mikakati
mbalimbali ambayo Bodi yake imekuwa ikitekeleza katika kuitangaza
Tanzania nje ya nchi kwa lengo kuvutia watalii wengi zaidi na kukuza
utalii kwa ujumla. Alitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni pamoja na
kuweka matangazo katika maeneo na vyombo mbalimbali vya habari nje ya
nchi, kualika na kuleta nchini watu maarufu ili kuja kutembelea vivutio
vyetu vya utalii, kuteua mabalozi wa hiari wa utalii na kutumia mitandao
mbalimbali ya kijamii.
Mkurugenzi Mwendeshaji Bibi Devota
Mdachi aliwakabishi mabalozi hao vielelezo mbalimbali vya utalii wa
Tanzania na kuahidi kuwa bodi yake itakuwa ikiwatumia vielelezo
mbalimbali vya utalii vitakavyo wasaidia katika kutekeleza jukumu la
kusaidia utangazaji utalii katika nchi walizopangiwa. Mabalozi hao
watano na nchi wanazokwendani Omari Yusuph Mzee (Algeria), Matilda
Masuka (Korea Kusini), Dkt. Pindi Chana (Kenya), Grace Mgovano (Uganda),
Fatma Rajab (Qatar) na Balozi Abdallah Kilima (Oman).
|






No comments:
Post a Comment