![]() |
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza
kwenye Mkutano wa mashauriano baina ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu
Majengo na Wakadiliaji Majenzi unaofanyika kwa siku mbili kuanzia jana,
katika Ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.
Judith Ferdinand, BMG
Bodi ya Usajili
wa Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi, nchini, imehimizwa
kushirikiana na wataalamu kutoka nchi jirani katika kutoa mafunzo kwa
wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi ili kuendane na teknolojia ya
kisasa.
Wito
huo umetolewa leo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mbarawa, katika mafunzo endelevu ya 27 ya Bodi ya Usajili wa
Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi yanayofanyika kwa siku mbili
katika ukumbi wa Rocky City Mall Jijini Mwanza.
Profesa
Mbarawa amesema,kwa kutumia wataalamu kutoka nje ya nchi, itasaidia na
kuwawezesha wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi, kubadilishana
uzoefu pamoja na kuendana na soko la ushindani.
Pia
amewaomba wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi,wanapopata fursa
katika miradi ya ujenzi watumie elimu walionayo, kwa ajili ya maslahi ya
taifa sambamba na uadilifu.
“mchina
na mturiki hawawezi kujua historia ya Tanzania lakini ninyi mnaijua
nchi yenu, hivyo zitumieni fursa zinapojitokeza katika kubuni michoro
ambayo itadumu zaidi ya miaka mia, kulingana na historia ya nchi,katika
miradi ya ujenzi,” amesema Profesa Mbarawa.
Hata
hivyo ameiomba, bodi hiyo kuhakikisha inasimamia na kufuata sheria
namba 4 ya mwaka 2010 katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi hasa kwa
wakaguzi wa majengo.
Kaimu Msajili wa Bodi, Albert Munuo, akizungumza kwenye mkutano huo.
Kaimu
Msajili wa Bodi hiyo, Albert Munuo, amesema lengo la mafunzo hayo ni
kuwaelimisha wataalamu na wadau wa sekta ya ujenzi kuendana na kasi ya
mabadiliko ya sayansi na teknolojia na kukabiliana na changamoto za
utandawazi, ili kuchangia kukuza uchumi wa nchi, ambapo mpaka sasa
yamewanufaisha wataalamu 5,556.
Mwenyekiti wa Bodi Dkt.Ambwene Mwakyusa, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Bodi, Mbunifu Majengo, Dkt.Ambwene Mwakyusa, amesema, sekta hiyo
inathamini jamii inayoitumikia hivyo wametoa vifaa vya maabara za
sayansi, vyenye thamani ya milioni 3, ili kuhamasisha vijana wanaosoma
masomo ya sayansi, kuja kusomea ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi.
Mwenyekiti wa Bodi Dr Ambwene Mwakyusa (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) vifaa vya maabara.
Aidha
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema vifaa hivyo atavipeleka
katika shule moja ya wasichana ya sayansi, sambamba ameishukuru bodi
hiyo kupitia wataalamu wa ujenzi kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitakua
chachu kwa wanafunzi kusoma masuala ya ubunifu majengo na ukadiriaji
majenzi.
|
March 23, 2017
WAZIRI MBARAWA AITAKA BODI YA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADILIAJI MAJENZI KUJITANUA ZAIDI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment