
Mratibu wa Mkutano Mkuu wa
Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh
akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia
Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha
vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini
Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson
Mandela.

AKIZUNGUMZA na waandishi wa
habari Mratibu wa Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa,
Tajiel Urioh alisema mkutano huo ni maigizo ya vitendo ya baraza kuu la
Umoja wa Mataifa ambapo vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 30 kutoka
sehemu mbalimbali wanapata fursa ya kujifunza Diplomasia, Uongozi na
namna Umoja Wa Mataifa unavyofanya kazi.
Bw. Tajiel Urioh alisema kuwa,
Mkutano huo unaojulikana kama kongamano kubwa kabisa la vijana nchini
linalowaleta pamoja vijana wadogo kutoka nchi mbalimbali tangu mwaka
1997. Aidha aliongeza kuwa Mkutano huo Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja
wa Mataifa utafanyika mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi
na Teknolojia ya Nelson Mandela kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi wa Mei
mwaka 2017, ambapo vijana takribani 200 kutoka katika nchi mbalimbali
wanatarajiwa kuhudhuria kujadili masuala yanayohusiana na Afya ya Uzazi
na Uzazi wa Mpango, Demokrasia na Amani katika nchi zinazoendelea,
Kuhama kuelekea kwenye Nishati safi na ya teknolojia mbadala na Elimu
kwa Maendeleo Endelevu.
Aliongeza kuwa majadiliano ya
mwaka huu yatajikita katika mada kuu: “Kuwawezesha Vijana katika
Diplomasia na Uongozi”. Mada hii inalenga kuwezesha ushiriki wa vijana
na kuwajengea uwezo kwenye masuala ya Diplomasia na Uongozi kwa kuwapa
mafunzo ya vitendo katika mada ngumu ambazo zitawaongezea ujuzi wa
majadiliano na kufikia muafaka wa masuala mtambuka yanayogusa maslahi ya
mataifa.
“Tunaishi katika ulimwengu ambao
diplomasia yenye ujasiri na uongozi vinahitajika sana hivyo basi
kuwakuza vijana katika uwanja huu itachangia kukua kwa mataifa yenye
watu wenye uwezo wa kuamua mambo yao. Katika mkutano wa mwaka huu
wajumbe watakuja na maazimio mbalimbali ambayo kwa namna moja hama
nyingine yatakuwa na manufaa katika maisha yao ya kila siku na watu
wanaowazunguka katika jamii zao,” alisema Bw. Urioh.

Mratibu wa Mkutano Mkuu wa
Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh
akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia
Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha
vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini
Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson
Mandela. Kushoto ni Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akiwa katika mkutano huo pamoja na
Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania,
Arafat B. Lesheoe.
“Ni matarajio yangu makubwa kwamba
mtakuwa tayari kujifunza kuendana na mada kuu ya ‛ Kuwawezesha Vijana
katika Diplomasia na Uongozi′ lakini pia kubadilishana mawazo na wajumbe
wengine na kutengeneza mtandao wa vijana wenye fikra mnazoendana nazo,”
aliongeza Tajiel Urioh, Mratibu wa Kitaifa wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa
wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2017.
Ofisa Habari wa Kituo cha Habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo alisema kongamano kama hilo
la vijana lina umuhimu mkubwa kwa vijana kwani huwajenga vijana kupitia
Club za UN. Aliwataja miongoni mwa vijana ambao ni matunda ya Club za
UN ni pamoja na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony
Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka, Balozi wa Tanzania
nchini Japan, Benedict Kikove, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum
Hapi, Mbunge wa Kibamba (Chadema), John John Mnyika na wengine wengi


No comments:
Post a Comment