Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama,
Viongozi wa CCM Kata ya Tabata, Jimbo la Segerea, wakati akiwa katika
ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Picha Zote
na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama,
Viongozi wa CCM Kata ya Tabata, Jimbo la Segerea, wakati akiwa katika
ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana.
Wanachana wa CCM Jimbo la Segerea wakiinua mikono kufurahia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo,jana.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama,
Viongozi wa CCM Kata ya Pugu, Jimbo la Ukonga wakati akiwa katika ziara
yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Mkutano huo
ulifanyika kwenye Ukumbi wa Check Point, Pugu.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama,
Viongozi wa CCM Kata ya Pugu, Jimbo la Ukonga wakati akiwa katika ziara
yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Mkutano huo
ulifanyika kwenye Ukumbi wa Check Point, Pugu.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama,
Viongozi wa CCM Kata ya Pugu, Jimbo la Ukonga wakati akiwa katika ziara
yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Mkutano huo
ulifanyika kwenye Ukumbi wa Check Point, Pugu.
Wanachama wa CCM Jimbo la Ukonga wamsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Rodrick Mpogolo,wakati
akiwahutubia kwenye Ukumbi wa Check Point jana.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akiwatambulisha Madiwani wa
Jimbo la Segera na kuwapa majukumu wakati wa mkutano huo.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, akizungumza jamabo na mmoja wa
wanachama wa CCM Kata ya Pugu wakati akiondoka baada ya kymaliza
mkutano wake katika Jimbo la Ukonga jana.
***********************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
UBABE
na unafiki wa baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) inaelezwa
kuwa ndio chanzo cha kupoteza jimbo la Ukonga na mengine ya Mkoa wa Dar
es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo, alisema hayo jana wakati
alipozungumza na wanachama na viongozi wa Chama katika majimbo ya Ukonga
na Segerea.
Alisema
viongozi hao waliendekeza mizengwe na umimi, ambapo matokeo yake
waliwavuruga wanachama na jimbo likachukuliwa na upinzani,sasa wanajuta.
“Tumewasababishia
wanachama kubaki kama wakiwa, hawana mbunge,na sehemu zingine hawana
madiwani. Yote ni kutokana na ubinafsi na makundi yaliyokiumiza
Chama,”alisema.
Mpogolo
alisema CCM haiwezi kukubali viongozi wachache wenye roho za chuki
waendelee kuwanyanyasa wanachama wenzao kwa sababu ya maslahi ya makundi
yao.
“Naomba kila mwanachana afanye mabadiliko ndani ya nafsi yake. Hatuna namna nyingine zaidi ya
kubadilika na kujenga taswira nzuri ya Chama chetu. Mtu anayeona hawezi kubadilika aende vyama
vingine,” alisema.
Aliwataka
viongozi na wanachama kuvua makoti ya zamani yaliyojaa chuki,roho
mbaya na ubinafsi na badala yake wavae makoti mapya ya upendo ,umoja na
mshikamano na kuingia kwenye timu ya ushindi ya CCM mpya na Tanzania
mpya.
Akiwa
katika jimbo la Segerea, Mpogolo aliwapongeza kwa kushinda jimbo hilo
na aliwapa pole kwa kupoteza kata zote za jimbo hilo,lakini aliwataka
wajitathmini maana wanajua nani aliyepoteza.
Mpogolo
alisema chanzo cha kupoteza kata zote 13 ni wana CCM walioamua kuuza
kata zote na kuwafanya wananchi wakose ‘connection’ Mwenyekiti wa Chama
Rais Dk. John Magufuli.
“Tumeweka
madiwani hawana hata mawasiliano na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa
Chama chetu. Hata kuwaletea maendeleo itakuwa ndoto kwa kuwa hawana
‘connection’na baba,”alisema.
Aliwataka
wanachama kuanza kujiandaa mapema kutafuta wafuasi kwa kujenga uhusiano
mwema na kuwa kishawishi kwa wananchi wengine ili kuongeza jeshi la
CCM.
“Ili ushinde unahitaji wafuasi wengi na uwe kivutio.Sasa kwa tabia zetu za figisu figisu, hasira
makundi, kushughulikiana tutawezaje kuvuta wafuasi.Ndio maana nawataka mbadilike ndani ya nafsi zenu,”alisema.
Akizungumza
kwa mifano Mpogolo alisema baadhi ya viongozi wamekuwa vikwazo na
kuwakera wanachama mpaka wengine wanakimbia CCM jambo ambalo halina
nafasi katika awamu hii.
“Kama tumejaa chuki, kufukuzana, kuchafuana ,kupakana matope,hatutaweza kuwavutia wanachama wapya.
Wanaofitini wenzao na kufukuzana bila sababu za msingi hawana nafasi CCM,”alisema.
Awali
Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe,alisema jimbo la
Segerea ndio eneo pekee ambalo Chama kilipoteza kata zote na hailezeki
ilikuwaje maana mbunge aliyeshinda ni wa CCM Bona Kaluwa.
Alimuomba Mpogolo, awafunde wanachama wa CCM waondokane na mapepo yaliyosababisha wauze kata zote za jimbo hilo.
Kwa
upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joyce Kaugala ,alisema ziara
ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama ,itasaidia kuwajenga wanachama ili
uchaguzi ujao waweze kukomboa kata zote.











No comments:
Post a Comment