
Mshambuliaji
raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ameifungia Borussia Dortmund
goli la mkwaju wa penati la dakika za mwisho katika siku ya mwisho ya
msimu wa Ligi ya Bundesliga na kuwa mfungaji anayeongoza kwa kufunga
magoli 31.Katika mchezo huo wa jana Aubameyang alifunga magoli mawili
wakati Dortmund ikiifunga Werder Bremen 4-3, goli lake la kwanza akilipata
dakika tatu kabla ya mapumziko na la pili katika dakika ya
89.Aubameyang anakuwa mchezaji wa pili kutoka Afrika kutwaa tuzo ya
kiatu cha dhahabu nchini Ujerumani, baada ya Mghana Tony Yeboah kutwaa
tuzo hiyo mara mbili wakati akiichezea timu ya Eintracht Frankfurt
katika msimu ya 1992-93 na 1993-94.
Pierre-Emerick Aubameyang akibusu tuzo yake ya ufungaji bora
Pierre-Emerick Aubameyang akipongezwa na wachezaji wenzake kwa kutwaa tuzo hiyo




No comments:
Post a Comment