
Timu ya vijana chini ya miaka 17
ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye
michuano ya AFCON U17 baada ya kuifunga Angola kwa mabao 2-1 kwenye
mchezo wa Kundi B uliochezwa Uwanja wa L’Amittee mjini Libreville,nchini
Gabon.
Vijana wa Serengeti Boys ndio
walikua wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya sita kipindi cha
kwanza baada ya Kelvin Naftal kupasia kamba kwa kichwa akiunganisha
krosi ya Nickson Kibabage.
Dakika ya 18 Angola walisawazisha
bao hilo kupitia kwa Pedro baada ya kutumia vizuri makosa ya safu ya
ulinzi ya Serengeti Boys na kufanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa
sare kwa kufungana 1-1.
Kipindi cha pili Serengeti
waliongeza kasi kutafuta bao na kufanikiwa kufunga dakika ya 69 mfungaji
akiwa ni Abdul Suleiman baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Yohana
Mkomola.
Serengeti Boys imefikisha pointi 4
baada ya kupata pointi moja kwenye mchezo wa kwanza kufuatia kutoka
sare ya bila kufungana dhidi ya Mali ambao ndio mabingwa watetezi.
Pointi hizo zinaifanya Serengeti
kuwa kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano
hiyo kwani watahitaji ushindi au sare dhidi ya Niger kwenye mchezo wa
mwisho wa kundi B.
Endapo Serengeti Boys itafuzu
kucheza nusu fainali ya AFCON U17 itakua imefuzu pia kucheza fainali za
kombe la dunia kwa vijana wa U17 zitakazofanyika nchini India baadae
mwaka huu


No comments:
Post a Comment