
Wafanyakazi wote wa DStv wavaa
sare za Serengeti boys kama njia mojawapo ya kuwaunga mkono katika
ushiriki wao katika michuano inayoendelea ya kombe la Afrika kwa
wachezaji wa umri wa chini ya miaka 17 nchini Gabon.

Wakizungumzia hatua hiyo baadhi ya
wafanyakazi hao wamesema kuwa kwakuwa DStv imejikita kwenye kuwapa
wananchi burudani, na kwakuwa wanaonyesha michuano hiyo mubashara,
wameona ni ni vyema wakawaunga mkono Serengeti boys kwa njia ya ziada –
yaani kuvaa jezi zao kama kwa siku ambayo timu hiyo inacheza.
Wamesema wanatambua kuwa Serengeti
boys inatuwakilisha hivyo ni muhimu sana kuinga mkono hata kwa
kuishabikia tu hata kama hatupo uwanjani. “Tumeamua kuvaa sare za
Serengeti boys leo kama ishara ya kuwaunga mkono na kuwatakia kila la
heri katika michuano hii inayoendelea nchini Gabon” alisema Revina
Bandihai na kuongeza kuwa wana imani na matumaini makubwa sana kwa
Serengeti Boys kwani ni timu ambayo imeonyesha kiwango cha hali ya juu.

DStv inaonyesha mubashara michuano
hiyo na mechezo yote ya Serengeti boys inarushwa kwenye Supersport
Select inayopatikana kuanzia kufurushi cha DStv Bomba kw ash.19m975 tu
ikiwa kwenye Lugha yetu pendwa ya Kiswahili.
Leo Serengeti Boys inacheza na Angola saa 11.15 jioni Supersport Select DStv chaneli namba 233.


No comments:
Post a Comment