Rais wa Simba Evans Aveva
Katika
kile kinachoonekana ni kama kuzima shamrashamra za Yanga baada ya
kutangazwa kuwa bingwa baada ya klabu ya Simba kuonyesha vielelezo vyote
vinavyoonyesha kuwa Simba imetuma rufaa yake FIFA. Vyanzo Sport Hits na Bin Zubeiry
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIMBA
SC inasambaza vilelezo kwamba imepeleka malalamiko Shirikisho la Soka
la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudai
wapewe pointi tatu walizopokonywa, ambazo wakifanikiwa kurejeshewa
watakuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ligi
Kuu imefikia tamati leo na Yanga SC wametawazwa tena kuwa mabingwa kwa
wastani wao mzuri wa mabao licha ya kufungana kwa pointi na Simba SC, 68
kila moja baada ya mechi 30 za msimu.
Lakini
Simba wanataka waikumbushie Yanga machungu ya mwaka 2000 walipofanikiwa
kutwaa ubingwa kwa matokeo ya uwanjani, kabla ya baadaye aliyekuwa
Waziri wa Michezo, Profesa Juma Kapuya kuwapa pointi za mezani Mtibwa
Sugar wakawa mabingwa.
Nakala
iliyosainiwa na Katibu wa Simba, Hamisi Kisiwa inaonyesha barua hiyo
ilitumwa Mei 17 kwa njia ya Fax na nakala yake wakapewa TFF.
Ikumbukwe
madai ya msingi ya Simba ni kurejeshewa pointi tatu walizopewa na
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 72
baada ya kuikatia rufaa Kagera Sugar kwa madai ya kumtumia beki
Mohammed Fakhi akiwa anatumia adhabu ya kadi za tatu njano.
Simba
SC ilifungwa 2-1 katika mchezo huo uliofanyika Aprili 2, mwaka huu
Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, lakini Kamati ya Saa 72 ikawpa pointi tatu za
mezani. Hata hivyo, Kagera Sugar wakakata rufaa TFF wakisema mchezaji
wao hakuwa ana kadi tatu, bali mbili na wakarejeshewa pointi zao.
Simba
nao sasa wameamua kusonga mbele hadi FIFA ili warejeshewe pointi zao na
hatimaye kutimiza ndoto zao za kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya
kwanza tangu mwaka 2012.






No comments:
Post a Comment