Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, (kushoto), akiwa amekamata fedha, ambazo ni rambirambi alizokabidhiwa na wawakilishi wa chama cha
wamiliki na wauza mafuta
rejareja Kanda ya Kaskazini, (TASDOA), Bw.Tinno Mmasi (katikati), na Bw.Deipyen
Bameda, ofisini kwake mjini Arusha.Rambirambi hizo ni kwa ajili ya
wanafunzi 32, walimu wawili na eeva wa shule ya msingi Lucky Vincent
waliofariki katika ajali ya barabarani huko Karatu.
Dare salaam
Independent School (DIS) Anna Msangi akiwa anakabidhi kiasi cha
shilingi milioni tatu kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ikiwa ni
mchango wao kwa wanafunzi wa Lucky
Vicent
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifafanua
jambo ofisini kwake kabla ajapokea rambirambi
hizo
Habari picha
na Woinde Shizza,Arusha
Baadhi ya
Wanasiasa
wametakiwa kuacha mara moja kuchulia
tukio la vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent kama sehemu yao ya
kujinufaisha kisiasa, pamoja na baadhi yao kupotosha jamii
kupitia mitandao ya kijamii .
Hayo
yamebainishwa jana na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
wakati alipokuwa akipokea rambirambi
za wanafunzi 32 wa Lucky Vicent,zilizotolewa
na chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja (TASDOA)
pamoja na uongozi wa shule binafsi ya Dare salaam
Independent School (DIS) ambapo alisema kuwa anasikitishwa sana na baadhi ya
viongozi kuchukulia swala hili kama ni sehemu ya kujijengea
umaarufu.
Alisema kuwa
swala hili sio tukio la kisiasa bali ni mtihani
na changamoto kubwa iliyozikumba familia za wananchi wa Arusha ,hivyo
linatakiwa kuheshimika na kuchukuliwa kama ni tatizo kubwa lililowakumba
wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kwani kuwapoteza watoto hawa
ni jambo la kusikitisha sana kwani walikuwa
wanategemewa kuwa viongozi wa baadae.
“pia napenda
kuchukuwa fursa hii kuwashukuru kwa kuleta
michango yenu kwa ajili ya wanafunzi hawa 32 ila napenda pia kuwakumbusha
kuwa jumla ya watu wote waliopata tatizo
walikuwa 38 lakini kati yao waliokufa ni 35 na
na wingine watatu ni majeruhi hivyo napenda kuwasihi wananchi na
mashirika ambayo wanaleta msaada wasiangalie waliopoteza maisha tu bali
wawakumbuke na wale majeruhi watatu ambao wapo nje kwa matibabu kwani wao pia
ni binadamu”alisema Gambo
Alisema kuwa
japo kuwa majeruhi wale waliopelekwa nje
kutibiwa wanaudumiwa bure lakini kuna wale watu ambao wameenda nao pamoja ya
kuwa wanahudumiwa chakula na malazi lakini kwa binadamu waka waida anatakiwa
kujitegemea kwa vitu vidogovidogo hivyo ni vizuri kama watu wanaotoa msaada
wata wakumbuka na hawa majeruhi .
Kwa upande
wake katibu mku u wa chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja
(TASDOA) Tino Mmasi alisema kuwa wao kama wamiliki wawauza mafuta wadogowadogo
wameguswa sana na msiba huu na ndio maana walioamua kukaa kama wanachama na
kuchanga fedha hizi kiasi cha shilingi millioni saba laki saba
ili ziwafariji wafiwa hawa 35 na pia wameaidi
kwend a kujichanga tena kwa ajili ya
kuwachangia majeruhi ambao wapo Marekani
“tumetoa hiki
kidogo lakini kwa jinsi tulivyoguswa tutaenda kuchanga fedha
zingine
kwa ajili ya majeruhi waliopo marekani na tunapenda kukuaidi mkuu wa mkoa
tutakuwa nanyi bega kwa bega hadi majeruhi hawa wote wapone na warudi hapa
nchini”alisema Mmasi


No comments:
Post a Comment