KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 22, 2017

KOZI YA WAAMUZI YASOGEZWA MBELE

unnamed
Kozi ya waamuzi wa mpira wa miguu, iliyolenga kuwainua  madaraja kutoka madaraja waliyonayo sasa hadi ngazi moja juu, imesogezwa mbele kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Saloum Chama.
Chama amesema kwamba kozi hiyo iliyopangwa kufanyika kuanzia Juni 29, mwaka huu itafanyika hapo baadaye katika tarehe itakayopangwa, lakini itakuwa ni kabla ya  Uchaguzi Mkuu wa TFF.
“Watu wasiende kuripoti hiyo Juni 29, mwaka huu kama tulivyotangaza. Tumesogeza mbele kidogo kozi hii. Tarehe mpya itatangazwa hapo baadaye,” amesema Chama ambaye alitaja vituo vilivyopangwa kuwa ni Mwanza, Ruvuma na Dodoma

No comments:

Post a Comment