Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetangaza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Chama
cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), utafanyika Agosti 05, mwaka huu mjini
Sumbawanga.
“Napenda kuwatangazia wadau wote
wa RUREFA kuwa mchakato wa uchaguzi utaendelea kuanzia pale ulipokomea,”
alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli
mara baada ya kikao cha Kamati hiyo, kilichoketi Juni 10, mwaka huu.
Wakili Kuuli amesema uchaguzi
utaendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA, kwa kusimamiwa na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF kama ilivyoanishwa kwenye taarifa ya awali.
Sasa kinachofuata ni kipindi cha
kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea ambapo zoezi hilo litafanyika
Julai 4 na 5, 2017 wakati Julai 6 na 7, mwaka huu itakuwa ni kupitia
pingamizi zote na kufanya usaili wa wagombea.
Kwa mujibu wa ratiba
iliyotangazwa, Julai 8, mwaka huu itakuwa ni hatua ya kutangaza na
kubandika kwenye mbao za matangazo matokeo ya awali ya usaili ilihali
Julai 9 na 10, mwaka huu Sekretariati kuwasilisha masuala ya kimaadili
kwenye kamati ya Maadili.
Kuanzia Julai 11 hadi 13, mwaka
huu itakuwa ni kipindi cha kupokea na kusikiliza na kutolea maamuzi
masuala ya maadili wakati Julai 14 na 15, mwaka huu ni kutangaza matokeo
ya uamuzi wa Kamati ya Maadili huku Julai 16 na 17, itakuwa ni kipindi
cha kukata Rufaa kwa maamuzi ya masuala ya kimaadili kwenye kamati ya
rufaa ya maadili ya TFF.
Julai 18 na 19, mwaka huu itakuwa
ni kipindi cha kusikiliza rufaa za kimaadili wakati Julai 20 na 21 ni
kutoa uamuzi wa Rufaa huku Julai 22 na 23, ni kipindi cha kukata rufaa
dhidi ya Kamati ya Uchaguzi kwenye kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Julai 24 hadi 26, ni kipindi cha
kusikilizwa rufaa kazi itakayofanywa na Kamati ya rufaa ya Uchaguzi ya
TFF ilihali Julai 27 na 28, ni kwa wagombea na kamati ya uchaguzi
kujulishwa maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Julai 29 na 30, mwaka huu ni
kuchapisha orodha ya mwisho ya wagombea na kutangazwa na kubandikwa
kwenye mbao za matangazo wakati kipindi cha kampeni kwa wagombea
kitakuwa ni kati ya Julai 31 hadi Agosti 4, mwaka huu. Uchaguzi Mkuu wa
RUREFA utakuwa Agosti 5, mwaka huu.
Hatua za awali zilizofanyika,
kabla ya kusimamishwa uchaguzi kutangaza mchakato wa Uchaguzi wa TFF
nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za matangazo; kuchukua na
kurudisha fomu za kuomba uongozi; hatua ya mchujo na kuchapisha na
kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea
No comments:
Post a Comment