KLABU ya Coastal Union ya Jijini
Tanga, imezika tofauti walizokuwa nazo awali zilizosababisha timu hiyo
ishuke kutoka Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa mwaka 2014/ 2015, na
sasa timu hiyo imeunda umoja wa viongozi utakaokuwa na lengo la
kuirejesha Ligi Kuu msimu ujao.
Akizungumza
jana kwenye mkutano wa wanachama uliofanyika makaomakuu ya klabuhiyo
barabara ya 11 Jijini hapa, Mwenyekiti wa kamati ya mashindano, Ahmed
Hilal ‘Aurora’ alisema kutokana na kikao kilichofanyika katika hoteli ya
Mkonge, kimezika tofauti hizo na sasa wapo pamoja.
Alisema
miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano huo uliorudisha umoja ni
pamojana Nassor Binslum ambaye ataisaidia tena kalbu hiyo pamoja na watu
wengine ili kuhakikisha timu hiyo itakayoshiriki Ligi Daraja la kwanza
iweze kurejea Ligi Kuu.
“Mkutano
uliofanyika Mkonge Hoteli umezika yote yaliyotokea na tumeunda umoja
ambao umewezesha timue yetu kusajili wachezaji watakaokuwa na uwezo wa
kupanda daraja…Tunachotaka sasa watu wote wajali Coastal kwanza mambo
mengine baadaye,” alisema Aurora.
Coastal
iliteremka daraja baada ya viongozi kuhitafiliana na Aurora akiwa
Mwenyekiti aliyeipandisha daraja timu hiyo msimu wa 2011-2012 alijiuzulu
wadhifa huo na baadaye timu kufanya uchaguzi uliomweka madarakani Dkt
Ahmed Twaha ambaye aliishusha daraja akiwa na katibu wake Kassim
El-Siagi na Akida Machai.
Mgogoro
huo ulisababisha baadhi ya watu kwenda kujiunga na timu ya Mgambo JKT
ambayo nayo ilishuka daraja hadi la kwanza huku wanachama wengine
wakienda katika timu hiyo ambapo zote mwaja jana zilizoposhiriki ligi
daraja la kwanza hazikufanya vizuri.
“Tumesamuheana
kabisa na sasa tupo pamoja, tusianze kunyoosheana vidole na kufukua
makaburi yaliyipita hatutafika tunapotaka kwenda lakini lazima mkumbuke
mpira sasa ni fedha…Nawakumbusha pia lipeni ada zenu muwe na sauti kwa
viongozi hawa,” alisema Aurora.
Makamu
Mwenyekiti wa timu hiyo Mohamed Musni, alisema kwamba hivisasa uongozi
wa klabu hiyo umepanga kuhakikisha inafanya vizuri katika Ligi daraja la
kwanza itakayoanzamwezi ujao ili wawqeze kurejea kwa kishindo Ligi Kuu.
Mjumbe
wa kamati ya utendaji ya timu hiyo Abdallah Zuberi ‘Unenge’, aliwataka
wanachama kuhakikisha wanaacha majungu ya kupeleka habari
zitakazowarudisha kule walipotoka na badala yake wahubiri umoja kwa
faida ya timu hiyo.
Kaimu
Katibu Mkuu Nassoro Kibabedi, aliwataka wanachama waisaidie timu hiyo
katika kipindi hiki na kamwe wasibweteke wakiamini kwamba wafadhili
watafanya kila kitu hivyo walipeada zao ili ziweze kuisaidia klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment