Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania bara Yanga wamemaliza Kambi yao Visiwani Pemba kwa
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jamhuri mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na
msimu pamoja na Mechi ya Ngao ya Hisani utakaowakutanisha na mahasimu
wao Simba Agosti 23 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Wakicheza katika uwanja wa Gombani
uliopo visiwani humo Yanga walipata bao hilo kupitia kwa beki wao wa
kushoto,Mwinyi Hajji kwa shuti kali lililoenda moja kwa moja na unakuwa
ushindi wa tatu wakiwa Zanzibara na ukiwa wa pili visiwani Pemba baada
ya Jumatano kuwafunga timu ya Chipukizi bao 1-0 ambalo lilifungwa na
Ibrahim Ajibu.
Baada ya hapo walipita visiwani
Unguja na kucheza na Mlandege na kupata ushindi wa jumla ya mabao 2-0
yakifungwa na Ibrahimu Ajibu na Emmanuel Martin huku kocha Mkuu George
Lwandamina akianza na vikosi viwili kipindi cha kwanza kilikuwa hiki
Kabwili, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Abdallah Hajji ‘Ninja’, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’/Pato Ngonyani dk34, Maka Edward, Pius Buswita, Said
Juma ‘Makapu’, Amissi Tambwe/Said Mussa dk34, Matheo Anthony na Juma
Mahadhi/Yussuf Mhilu dk34.
Kipindi cha pili Yanga walifanya
mabadiliko kwa kukitoa kikosi kizima na kuingiza hiki Youthe Rostand,
Hassan Kessy/Juma Abdul dk70, Gardiel Michael, Kevin Yondan, Andrew
Vincent ‘Dante’, Papy Kabamba Tshisbimbi, Thabani Kamusoko, Donald
Ngoma, Ibrahim Hajib, Emmanuel Martin na Raphael Daudi.
Hata hivyo hakikuweza kubadili
matokeo na kubaki kuwa bao moja hilo na kujiweka mguu sawa kuwavaa
watani wao wa Jadi Simba kwenye ngao ya hisani Mchezo unaotarajiwa kuwa
na upinzani Mkubwa hii inatokana na usajili uliofanywa na timu hizo.
Yanga wanatarajia kuingia jijini
Dar es salaam Siku ya Jumanne ya wiki inayoanza kesho tayari kwa vita ya
Ngao ya Hisani pamoja na kuanza Mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Tanzania
bara linalotanzamiwa kufunguliwa Agosti 26 huku Mabingwa hao watetezi
wakitaraajia kutupa karata yao siku ya Jumapili ya Agosti 27 kuvaana na
wageni wa Ligi timu ya Lipuli FC kutoka Iringa.
No comments:
Post a Comment