Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisaini
Mkataba wa Makubaliano kati ya Tanzania na Afrika Kusini wa namna ya
kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kwa lengo la
kukusanya, kuhifadhi, kuendeleza na kuzitunza urithi huo kwa manufaa ya
kizazi cha sasa na vizazi vijavyo mjini Dodoma jana Tarehe 19 Septemba
2017. Kushoto ni Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Afrika Kusini Mhe. Nathi
Mthethwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia)
akibadilishana Mkataba wa makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi
wa Ukombozi wa Bara la Afrika na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika
Kusini Mhe. Nathi Mthethwa mara baada ya kusaini mkataba huo mjini
Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017.
Waziri wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akiongea na viongozi kutoka Tanzania na Afrika Kusini waliohudhuria
hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya
Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika mjini Dodoma jana Tarehe 19
Septemba 2017.
No comments:
Post a Comment