KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 17, 2017

IMAMU AWAKATAZA WAUMINI KUBOMOA MSIKITI

Imamu wa Msikiti wa Al Masjid Kirumbi Islamic Center uliopo Kimara amewazuia waumini wake kutoshiriki katika kuvunja au kutoa kitu chochote katika msikiti huo ambao unatakiwa kuvunjwa na Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS.



Imamu wa Msikiti huo Ramadhan Juma  amesema hayo jana  wakati akifanyiwa mahojiano na MCL na kudai kutokana na imani yao ni kosa kubwa mtu yoyote kuvunja nyumba ya ibada kwa kuwa hiyo ni nyumba ya Mungu na kusema wao hawajatoa kitu chochote zaidi ya vitu vidogo ambavyo vinatumika kusaidia jamii kama jeneza.



"TANROADS wametupa barua ya kuvunja msikiti ndani ya wiki moja kwa kile wanachodai umevamia eneo la barabara hivyo walitaka tutoe vifaa ndani ya wiki moja kupisha zoezi la barabara lakini kutokana na imani yetu na Uislam unavyotufundisha ni kosa kubwa kuvunja nyumba ya 'Allah Subhanahu Wa Ta'ala' 



"Hii ni nyumba ya ibada hivyo hatutainua mikono yetu kwa kujihukumu sisi wenyewe kwa amri ya dini yetu ya Kiislam kwetu sisi ni kosa mtu kutoa mkono wake kutoa sijui bati au chochote kile kinachohusu msikiti kwa hiyo ndiyo maana tumeshindwa kuvunja msikiti huu" alisisitiza Imamu Ramadhan



Hata hivyo Imamu alisisitiza kuwa wao wameiachia serikali na hao TANROADS waweze kubomoa wenyewe na kusema yeye amewakataza waumini wake wasishiriki cha chochote katika kubomoa nyumba hiyo ya ibada



"Nimewaambia waumini wangu wasitoe chochote katika kuvunja kwa msikiti huu, tutatoa vitu vidogo vidogo ambavyo vinasaidia jamii kama vile jeneza na vinginevyo tumevitoa lakini katika majengo kwa chochote kile tunawaachia wenyewe, hii ni nyumba ya Allah hivyo wavunje wao halafu Mungu mwenyewe ndiye atajua kwa kuwa hiyo ni nyumba yake atakavyohukumu yeye ndiye anajua kwa kuwa hiyo ni nyumba yake" alisema Imamu Ramadhan Juma

No comments:

Post a Comment