KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 23, 2018

HALMASHAURI ZAPIGWA 'STOP' KUCHUKUA MAENEO YA WANANCHI BILA FIDIA

     Serikali imepiga marufuku halmashauri kuchukua maeneo ya wananchi bila ya kuwalipa fidia, kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria ya nchi.
     Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula wakati akizungumza Wilayani Butiama mkoa wa Mara katika ziara yake ya kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi.
Waziri Mabula amezisisitiza halmashauri hizo kufanya mazungumzo na wananchi husika kabla ya kuchukua maeneo yao.
     “Wakati wa mchakato wa kuchukua maeneo ya wananchi ni vyema wahusika wakashirikishwa kuanzia hatua ya awali pamoja na kuelimishwa juu ya zoezi hilo ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea,” amesema.
     Katika hatua nyingine, Mabula ameziagiza halmashauri hizo kuzingatia mipango miji ili kuwe na miji bora.   

No comments:

Post a Comment