CHAMA
cha Wananchi (CUF) mkoani Mwanza kimempiga marufuku Katibu Mkuu, Maalim
Seif Sharif Hamad kutofanya mikutano na vikao vya kisiasa katika wilaya
za Nyamagana na Ilemela zilizoko jijini hapa.
Hatua
hiyo ya kumpiga marufuku Maalim Seif aliyesimamishwa uongozi na Baraza
Kuu la Uongozi la CUF Taifa, imetolewa katika tamko la pamoja la
viongozi katika wilaya za Ilemela za Nyamagana mkoani Mwanza.
Viongozi
hao waliongozwa na Mwenyeviti wa CUF wa Wilaya ya Nyamagana, Salum
Mkumbukwa aliyekuwa ameambatana na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi
Taifa, Martha Haule na Zainabu Ally.
Walidai
kuwa wamesikia kuwa Maalim Seif anawasili jijini Mwanza kwa siri
kupitia mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa lengo la
kuhudhuria kongamano moja la chama cha siasa linalotarajiwa kufanyika
hivi karibuni katika wilaya za Nyamagana na Ilemela akiwa na lengo la
kukutana na wanachama wa CUF, jambo ambalo uongozi halina tija kwa
wakati huu wakati akiwa amesimamishwa uongozi.
Viongozi
hao walisema wamemwandikia barua Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na wakuu wa wilaya za Nyamagana na Ilemela
kupinga ujio wake.



No comments:
Post a Comment