Serikali
ya Marekani imeweka kipingamizi juu ya muswada ulioletwa na Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) Jumamosi ukitaka uchunguzi ufanyike juu
ya Israeli kutumia risasi za moto dhidi ya Wapalestina walioshiriki
katika maandamano katika Ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa maelezo ya
mwanadiplomasia wa Baraza hilo ambaye alilifahamisha shirika la habari
la Ufaransa.
Vyombo
vya usalama vya Palestina vimesema kwamba sio chini ya watu 15
waliuwawa Ijumaa na majeshi ya Israeli na zaidi ya watu 750 walitupiwa
risasi za moto.
Wapalestina walizika maiti za watu wao Jumamosi, huku waombolezaji wakitangaza kulipiza kisasi.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamini Netanyahu aliyapongeza majeshi ya Israeli ambayo yalitupa risasi dhidi ya Wapalestina.
“Hongereni askari wetu,” waziri mkuu alisema katika tamko la serikali. “Israel inachukua hatua thabiti na kwa azma ya kulinda uhuru wake na usalama wa wananchi wake.”
Wapalestina walikuwa katika siku ya maombolezo ya kitaifa Jumamosi.
Shirika
la habari la Associated Press (AP) limeripoti Jumamosi kuwa mmoja wa
waandishi wake walishuhudia Wapalestina wawili, katika matukio mawili
tofauti, ambao walikuwa wakitembea karibu na mpaka wa eneo lenye uzio la
Ukanda wa Gaza linalotenganisha Israeli kutoka kwa Wapalestina.
Wanajeshi wa Israeli waliwatupia risasi na kuwapata Wapalestina hao
miguuni.
Katika
tukio jingine, kijana wa miaka 16 ameiambia AP yeye alitupa mawe
kuelekea katika mpaka huo siku ya Ijumaa na kutupiwa risasi zilizolenga
miguu yote miwili. Kijana huyo alikuwa hospitali akitibiwa wakati mguu
mmoja umefungwa bendeji na mwengine umetiwa vyuma, wakala wa habari
wameripoti.



No comments:
Post a Comment