Nchi
ya China Ijumaa hii imeionya Marekani kuwa haiogopi vita vya kibiashara
wakati huu ikitishia kutoza kodi ya zaidi ya dola bilioni 3 kwa bidhaa
kutoka nchini Marekani katika kile kinachoonekana kujibu tangazo la rais
Donald Trump kutoza kodi dhidi ya bidhaa kutoka China.
Utawala
wa Beijing umetoa orodha ya bidhaa ambazo zitalengwa na kuongezewa
ushuru wa hadi kufikia asilimia 25 kuanzia kwenye matunda hadi kwa nyama
ya nguruwe licha ya kuwa imeshindwa kuchukua hatua zaidi na kuonesha
nia ya kuwa na mazungumzo.
Hatua
za hivi karibuni zimeshuhudia masoko ya hisa yakiporomoka wakati huu
Marekani, ambayo inaituhumu Uchina kwa wizi wa haki miliki pamoja na
hatua nyingine ambazo sio za haki dhidi ya makampuni yake, huenda
ikachochea vita ya kibiashara.
"China haitaki kupigana vita ya kibiashara, lakini haiogopi kabisa vita hiyo," imesema taarifa ya wizara ya biashara ya China.
Mapema rais Donald Trump alitia saini amri ambayo itaweka ukomo kwa uwekezaji wa makampuni ya Uchina nchini humo.
"Tuna
tatizo kubwa la wizi wa haki miliki linaloendelea kwa sasa," amesema
rais Trump wakati akitia saini agizo hilo ambalo litajumuisha bidhaa
ambazo zitatozwa ushuru wa hadi kufikia asilimia 25.
Hatua
ya Trump haijachukua mara moja hatua za kuweka ushuru mpya, lakini
ndani ya majuma mawili waziri wa biashara wa Marekani anatarajiwa
kutangaza bidhaa zilizolengwa kwenye amri hiyo ya rais Trump.
Wakati
huu rais Trump akionekana kutafuta ugomvi na mataifa yenye nguvu,
utawala wa Beijing umeonya kuwa vita vya kibiashara havitamnufaisha
yeyote na haitakaa kimya kuona Marekani ikitoa adhabu kwa biashara zake.
Waziri
wa viwanda Wilbur Ross alisema Alhamisi ya wiki hii kuwa hatua za
kulinda haki zake miliki ililenga kuifanya China ije kwenye meza ya
mazungumzo na kujadiliana kutafuta njia za kudhibiti wizi huo.
No comments:
Post a Comment