Meya
Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa, Machi 21, 2018 kwenye kikao cha
robo ya pili ya Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam ,ambapo
amewaeleza madiwani hao kuwa jukumu la kuzika marehemu wasiokuwa ndugu
ni la jiji, kwakushirikiana na halmashauri hivyo wanapaswa kuwajibika
katika hilo.
Amefafanua
kuwa hadi sasa jiji limeshanunua gari pamoja na mahitaji mengine ya
kuhifadhia miili hiyo pindi inatokea na kwamba changamoto iliyopo ni
watu ambao watashirikiana kutekeleza jukumu hilo.
“
Mtakuabliana na mimi kwamba tulishakubaliana kwamba jambo hili
lifanyike kwenye halmashauri zetu, lakini hadi sasa Kinondoni pekee ndio
wametimiza agizo hili, sasa ninaagiza tena halmashauri nyingine za jiji
hili kuajiri watu hao” amesema Meya Mwita.
Mwita
amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na halmashauri
nyingine zilizopo jijini hapo walikubaliana kuzika watu wasiokuwa na
ndugu hivyo kila mmoja anapaswa kutekeleza makubaliano hayo.
“Hivyo
marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzikwa na jiji,
natulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda,” amesema.
Amefafanua
kuwa watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa, wanapokaa hospitalini zaidi ya
siku 20,jiji linalazimika kuwazika hivyo wapo ambao wanazikwa kwenye
halmashauri mbalimbali.
Hivyo
wakati Jiji la Dar es Salaam likitimiza wajibu wake katika kuzika
marehu hao kila halmashauri linajukumu la kutoa watumishi kwa ajili ya
kuzika.
Amefafanua
taarifa alizonazo ni Halmashauri ya Kinondoni pekee ndio ambayo
imeajiri watumishi kwa ajili ya kuzika miili ya watu ambao wamefariki na
hawana ndugu.
“Ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha wanafanikisha kupatikana kwa watumishi hao haraka,” amesema Meya Mwita.
No comments:
Post a Comment