Victor
Kimesera, mmoja wa waasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa
anapatiwa matibabu.
Uongozi wa juu wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini umesema umepokea kwa mshituko taarifa ya msiba huo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti
wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, Kimesera alifariki dunia usiku wa
kuamkia juzi.
“Chadema
tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za msiba huu. Tumeondokewa na moja
ya nguzo muhimu za ustawi wa chama chetu ambaye amekuwa katikati ya
mapambano tangu aliposhiriki kuasisi chama hiki hadi umauti ulipomkuta
akiwa mtendaji wa chama makao makuu,” Mbowe alisema katika taarifa hiyo.
“Kimesera
maarufu kama VPK kama tulivyozoea kumuita, ametutoka katika kipindi
ambacho mchango wake ungehitajika sana, hasa wakati huu ambapo taifa
letu linapita katika mkwamo mkubwa wa kisiasa.
Atakumbukwa
zaidi kwa namna alivyojitolea kwa hali na mali kupigania haki,
demokrasia na maendeleo nchini na kipekee katika Jimbo la Kiteto mkoani
Manyara.”
Katika
taarifa yake hiyo, Mbowe alisema kwa sasa chama kupitia ofisi ya Katibu
Mkuu kinashirikiana na familia ya marehemu kuhusu taratibu mbalimbali
za msiba huo na ratiba ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es
Salaam zitatolewa baadaye.



No comments:
Post a Comment