Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii, Nape Nnauye
amesema anatamani bunge lisiwe la kutunga sheria tu bali pia lifute
sheria za hovyo au kuzirekebisha.
Pia
Nape ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya uchambuzi wa
sheria zake na kuangalia namna ya kuondoa sheria kandamizi katika sekta
ya utalii ili taifa linufaike na rasilimali zilizopo katika sekta hiyo.
Akizungumza
katika kikao cha kamati hiyo Mjini Dodoma leo Jumatano Machi 28, Nape
amesema zipo sheria ambazo ni kandamizi hivyo wizara inapaswa
kuzichambua na kupeleka bungeni ili ziondolewe au zifanyiwe marekebisho.
“Fanyeni
uchambuzi wa sheria kandamizi, mi natamani bunge lisiwe la kutunga
Sheria tu ,bali pia lifute Sheria za hovyo au kuzirekebisha,” amesema
Nape.
Aidha,
ameitaka wizara hiyo kuongeza vigezo vya kupima madhara ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) katika sekta ya utalii lakini pia kutoa
taarifa ya uchambuzi wa kodi mbali mbali katika wizara hiyo.
“Naomba
tusijpe muda mrefu wa kupima madhara ya VAT, wenzetu Kenya wameshafuta
hiyo, sasa hadi wamefuta wao si wajinga,” ameeleza.



No comments:
Post a Comment