Askofu
Wilberforce Luwalira wa Kanisa la Roma la Mtakatifu Paulo, Namirembe
nchini Uganda alinusurika kifo baada ya Herbert Kadu (35), kuibuka
ghafla kanisani akiwa ameshika panga na kumkimbilia nalo madhabahuni
wakati ibada ya Pasaka ikiendelea.
Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi nchini Uganda wakati Askofu Luwalira akiendesha ibada ya Pasaka kanisani hapo.
Ujumbe
wa video fupi uliosambaa jana kwenye mitandao ya kijamii unaonyesha
ibada hiyo ikiendelea, ghafla Kadu akiwa amebeba panga alianza
kumkimbilia eneo la madhahabuni alikokuwa askofu huyo.
Kabla
ya kumfikia askofu huyo, Kadu alijaribu kuruka kizingiti
kilichotenganisha eneo la madhabahu na waumini na katika jitihada hizo
alianguka na kukamatwa na wasimamizi na waumini ndani ya kanisa hilo.
Kijana
huyo alijaribu kuruka kizingiti ili kwenda kwa askofu ambaye wakati huo
alikuwa amesimama na msaidizi wake wakiendelea na ibada, na baada ya
kuruka alidondoka upande wa madhahabu.
Wasaizidi wa askofu huyo walimdhibiti kijana huyo na kumbeba kumwondoa ndani ya kanisa hilo ili asitekeleze kusudio lake.
Taarifa
zilizopatikana kanisani hapo zilisema kijana huyo aliwasili kanisani
hapo akiendesha gari aina ya 'kipanya' Super Custom na kuegesha lango
kuu la kuingilia kanisani hapo.
“Alipoingia
alimpiga mlinzi wa getini na kuingia kwa nguvu kanisani na alikaa
kanisani muda mrefu hadi ibada ilipokaribia kuisha ndipo alipojaribu
kwenda madhabahuni,” shuhuda alisema katika video hiyo.
Taarifa ilisema baadaye askari walimkamata na kumpeleka kituo cha polisi Namirembe kwa mahojiano.



No comments:
Post a Comment