Bunge
limeitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kufanya ukaguzi
polisi, magerezani na sehemu nyingine zinazolalamikiwa kuvunja haki za
binadamu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa,
alisema hayo Jumatano Aprili 18, wakati akisoma maoni ya kamati yake
kwenye mapato na Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria.
“Kwa
kuwa kumekuwapo na malalamiko mengi kuhusu uvunjwaji wa haki za
binadamu, ukiukwaji wa misingi kuhusu utawala bora nchini pamoja na
tuhuma za kushikiliwa watu magerezani, polisi na sehemu nyinginezo
nchini, pasipokuwepo utoaji haki au majibu yanayoridhisha.
“Kamati
inashauri tume ifanye ukaguzi katika sehemu zote nchini zenye
malalamiko hayo na kutoa taarifa kwa mujibu wa sheria ili kutatua
changamoto hizo endapo zitabainika kuwepo,” alisma Mchengerwa.
Kamati
hiyo pia ilishauri Tume ya Utumishi wa Mahakama, kutatua changamoto ya
mahakimu na kuhamishwa vituo na kupandishwa vyeo bila kulipwa stahiki
zao kwa wakati.
Kwa
upande wa Kamati ya Bajeti, Mchengerwa amesema kati ya fedha
zinazoombwa kwa mwaka 2018/19, ikilingishwa na zile za 2017/18, matumizi
mengineyo zimeongezeka kwa asilimia moja, za maendeleo zimeongezeka kwa
asilimia 98 huku za mishahara zikipungua kwa asilimia 3.3.



No comments:
Post a Comment