Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu
Wallace Karia ameipongeza klabu ya Young Africans kwa kufanikiwa kuingia kwenye
hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Africa.
Young Africans imefanikiwa kuingia kwenye hatua hiyo kwa
ushindi wa jumla ya mabao 2-1 baada ya kushinda mchezo wao wa kwanza kwa mabao
2-0 kabla ya kufungwa bao 1-0 na timu ya Welaitta Dicha ya Ethiopia.
Rais wa TFF Ndugu Karia kwa niaba ya TFF ameipongeza klabu
ya Young Africans kwa hatua hiyo kubwa iliyofikia ambayo inaakisi mpira wa
Tanzania kiujumla.
“Mafanikio ya klabu ya Young Africans ni mafanikio ya
Tanzania kiujumla na TFF ambao ni wasimamizi wa Mpira nchini tunajivunia
mafanikio hayo ya Young Africans ambao tumekuwa tunashirikiana nao bega kwa
bega kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera ya Tanzania”amesema Karia.
Amesema anaamini watafanya maandalizi ya kutosha
kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye hatua hiyo ya makundi.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF


No comments:
Post a Comment