| Mkurugengi Mkuu wa Benki ya biasahara ya CBA hapa nchini Dk Gift Shoko, akizungumza wakati wa hafla hiyo. |
Huduma
ya M-Pawa inayotolewa na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) imetoa
mikopo yenye thamani ya Sh10 bilioni kwa wateja wake katika kipindi cha
miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.
Huduma
hiyo inayotolewa kwa ushirikiano kati ya benki hiyo na kampuni ya simu
ya Vodacom, imepata muitikio kutokana na Watanzania kufungua akaunti za
huduma hiyo mahali popote walipo kwa kutumia simu za mkononi.
Zaidi
ya wateja millioni 7 nchini wamejiunga na huduma hiyo ya M-Pawa na
kuwawezesha wananchi wengi kupata mikopo inayowasaidia kupambana na
umaskini.
Akizungumza
katika hafla ya siku ya wateja wa benki hiyo jijini Mwanza juzi,
Mkurugenzi wa benki hiyo, Gift Shoko alisema benki hiyo itaendelea
kuwekeza kwenye teknolojia ili kuwezesha upatikanaji wa huduma kwa
wateja pamoja na kuongeza kasi na ufanisi.
“Wananchi
lazima waendane na mabadiliko ya teknolojia ili kujikwamua kiuchumi
kama vile matumizi ya simu na mitandao ili kurajisisha upatikanaji wa
huduma za kibenki kupitia simu za mkononi na mitandao,” alisema
Aliongeza kuwa kupitia huduma ya M-Pawa wananchi wengi hawatumii muda mwingi katika kufuatilia mikopo kwenye benki.
Akizungumzia
ufungwaji wa matawi manne katika jiji la Dar es Salaam eneo la
Kariakoo, Mkurugenzi huyo alisema matawi hayo ya benki yalikuwa
yamekaribiana huku wakilenga kujikita katika kutoa huduma kwa njia ya
mtandao.
Mmoja
wa wateja waliohudhuria hafla hiyo, Julius Stephen aliiomba benki hiyo
kufungua matawi mengi mkoani Mwanza ili kurahisisha upatikanaji wa
huduma kwa wananchi.
Naye
meneja wa benki hiyo tawi la Mwanza, Adam Makaka alisema wanalenga
kuongeza kiwango cha utolewaji wa mikopo kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza
kutokana na kuwepo kwa biashara nyingi ndogondogo.


No comments:
Post a Comment